BREAKIIIIG NEWSSSSSS!!!!!!!!, MKUU WA WILAYA YA SERENGETI JAMES YAMUNGU AMEFARIKI DUNIA

Wakati wa uhai wake Juni 23, mwaka huu, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, James Yamungu akiaga mwili wa marehemu Willy Edward.

 Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, James Yamungu, amefariki mchana huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Yamungu ambaye Agosti 13, aliiupokea Mwenye wa Uhuru kutoka Mkoa wa Arusha, na kukimbizwa wilayani kwake, aliukabidhi akiwa salama salimini kwa wilaya ya Bunda Agosti 14.

Akielezea juu ya kifo hicho, Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa, alisema kuwa, Yamungu aliugua ghafla Agosti 16 na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Baada ya hali yake kuzidiwa katika hospitali hiyo,  alisafirishwa jana kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo leo amepatwa na mauti.

Juni 23, mwaka huu, Blog ya Kamanda wa Matukio alikutana na Yamungu wakati wa msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo leo, marehemu Willy Edward mjini Mugumu, Serengeti.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake.

Amina.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA