BREAKING NEWS ....NAIBU WAZIRI AFRIKA MASHARIKI APATA AJALI JIONI HII

Wananchi wakitazama gari la naibu waziri wa Afrika Mashariki





Mzimu wa ajali kwa wabunge na viongozi wa Taifa umeendelea kushika kasi hapa nchini baada Naibu waziri wa Afrika Mashariki,Abdullah Juma Abdalla Saddallah na familia yake kupata ajali mbaya eneo la Tumbi Kibaha wakati akitoka Bungeni na familia yake.

Ajali hiyo mbaya ilitokea majira ya jioni hii wakati naibu waziri huyo akitokea Bungeni kuelekea jijini D'salaam akiwa na mkewe pamoja na watoto wake wawili na a dereva wake ambaye aliumia vibaya na kukimbizwa hospital yaTumbi-KibahaMashuhuda wa ajali hiyo akiwemno Abdulaziz Video amedai kuwa chanzo cha ajali hiyo inasemekana alikuwa analikwepa Lori alilokuwa akipishana nalo na hivyo gari lake kuhama njia na kupinduka .

Imeelezwa baada ya ajali hiyo umati wa wananchi wakiwemo vibaka walifika eneo hilo kutaka kupora mali mbali mbali ila hawakuweza kufanikiwa baada ya raia wema kusaidia kuepusha hali hiyo .

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo baada ya kuhojia na mwandishi wa habari hizi na kuwa hali ya naibu waziri huyo si mbaya sana zaidi ya dereva wake ambaye ameumia kichwani."

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU