CHADEMA MKOANI IRINGA WAEPUSHA SHARI NA MALUMBANO WAAMUAKUSITISHA MKUTANO WAO LAKINI KUENDELEZA OPERESHENI YAO BAADA YA SIKU TANO

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwao akiongea na wanachama wa chadema jana iringa
Mkuu wa FFU mkoa wa Iringa afande Mnunka akiongea na Mbunge Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwao.
 Magari ya polisi yakiwa tayari kwa lolote baada ya mkutano wa chadema kuahirishwa jana jioni
 Msafara wa Chadema ukiwa na viongozi wa kitaifa wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema)ukiingia mjini Iringa wakitokea mkoani Morogoro.Picha na Denis mlowe
 
 
 
JESHI la polisi mkoa wa Iringa na chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wasumbuana kwa zaidi ya masaa 10 jana katika harakati za kuzuia mkutano wa chama hicho.
Chadema na polisi walijikuta katika mvutano mkali na kuzungushana huku na kule  baada ya viongozi wa Chadema mkoa wa Iringa kushikilia msimamo wao wa kuwepo kwa mkutano huo katika viwanja vya mwembetogwa pamoja na jeshi la polisi kuzuia mkutano huo.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia mvutano huo mkali baada ya askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiongozwa na kamanda wake Mnunka wakitanda eneo la uwanja wa mkutano eneo la Mwembetogwa huku viongozi wa Chadema wakizunguka huku na kule mjini Iringa kushinikiza mkutano huo.

Mbali ya askari hao kumwagwa eneo la uwanja wa Mwembetogwa na hata kuzuia wafanyabiashara ndogo ndogo eneo hilo kuondoka ,bado idadi kubwa ya askari walionekana wakizunguka maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa huku baadhi yao wakiwa wametanda nje ya ofisi ya Chadema wilaya ya Iringa mjini eneo la Mshindo kama njia ya kuzuia viongozi hao kutoka kwa maandamano eneo hilo.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwao (Chadema) ambaye pia ni mjumbe kamati kuu Taifa alisema kuwa kutokana na mvutano huo wa jeshi la polisi na Chadema wameamua kutoufanya mkutano huo jana
 
Abwao alisema kuwa kutokana na hoja hiyo ya polisi ya kuwa kwa sasa ni zoezi la sensa ya watu na makazi wamelazimika kutii agizo hilo na hivyo kuamua kusogeza mbele mkutano huo.

Hata hivyo alisema baada ya jeshi la polisi kutangaza kusitisha mkutano huo kwa upande wake alilazimika kutangaza katika vyombo mbali mbali vya habari zikiwemo radio za mkoa wa Iringa ili kusitisha mkutano huo japo tayari kulikuwepo na maandalizi makubwa ya mkutano huo.

Hata hivyo Abwao aliwaomba radhi wananchi wa jimbo la Iringa mjini ambao walikuwa tayari kushiriki mkutano huo na kuwaomba wajiandae kwa wakati mwingine ambao chama hicho kitatangaza mkutano huo ."Chadema tumetumia busara kuepusha shari zaidi kati ya polisi na chama pia kuepusha wananchi kumwaga damu"

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda alieleza sababu za kuzuia mkutano huo kuwa ni baada ya kupokea agizo kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa nchini hasa baada ya tukio la Morogoro juzi. Hivyo alisema kwa sasa wakati zoezi la sensa linaendelea chama chochote cha siasa hakitaruhusiwa kufanya mkutano wa hadhara hadi hapo zoezi hilo la Sensa litakapokamilika.
 
Askari polisi hao wakiongozwa na askari wa FFU zaidi ya 100 waliuzuia msafara huo eneo la Zebra katika barabara kuu ya Iringa - Dodoma baada ya jeshi hilo awali kuzuia maandamano ya Chadema na vyama vyote kwa maelekezo ya msajili wa vyama vya siasa.

Hata hivyo kutokana na umati mkubwa wa wananchi kufika eneo hilo viongozi wa Chadema na polisi waliweza kukubaliana msafara huo kuendelea na safari yake kuelekea nyumbani kwa mbunge Msigwa eneo la Kihesa .

Katika tukio hilo jeshi la polisi halijaweza kutumia mabomu wala nguvu zaidi katika kuwatawanya wananchi kama ilivyo kuwa mkoani Morogoro juzi na sasa msafara huo umeshawasili mkoani Iringa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.