Hongera Asah Mwambene


Kwa niaba ya Mtandao wa wanataaluma Tanzania (Tanzania Professionals Network- TPN) nachukua nafasi hii kumpongeza Mzalendo Asah Mwambene (41) kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo).
Kabla ya uteuzi huu Mwambene alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano , Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, pia aliwahi kufanya kazi TSN.

Mwambene ni Mzalendo wa kweli na ni mdau wetu muhimu katika kuleta maendeleo endelevu Tanzania na amekuwa akifuatilia na kushiriki shughuli zetu za TPN.

Ni matumaini yetu kuwa utatimiza wajibu wako vizuri na kwa weledi wa hali ya juu kwa kuzingatia misingi ya taaluma ya habari kwa manufaa ya watanzania  wote.
Kila la heri na Mungu akubariki.

PHARES MAGESA
RAIS - TPN
+255 784 618320
To join TPN download form at www.tpntz.org

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA