KAL;ALA JUNIOR AREJEA TWANGA



Mwanamuziki aliyejiunga na Twanga Pepeta akitokea bendi ya Mapacha Watatu, Kalala Junior akiimba nyimbo yake mpya Nyumbani ni Nyumbani wakati wa mkutano wa kumtambulisha kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kiongozi wa bendi hiyo, Saleh Kupaza.Kwa hisani ya Habari Mseto Blog





DAR ES SALAAM,Tanzania
UONGOZI wa kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET) umemtambulisha rasmi mwanamuziki mwenye vipaji vingi, Kalala Hamza Kalala maarufu kwa jina la Kalala Junior.
Kalala alitambulishwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Mango Garden ambapo mbali ya kusema kuwa amerejea kwa lengo la kuendeleza bendi yake hiyo aliyokuwa nayo kabla ya kujiunga na Mapacha Watatu.
Mwimbaji huyo maarufu alisema kwa fumbo kuwa “Koti limembana akiwa na bendi yake ya Mapacha na kuamua kulivua na kuacha kuendelea kulivaa tena” na kujiunga na Twanga.
“Nimefurahi kujiunga na Twanga tena na nimekuja na zawadi za nyimbo mbili, wimbo wa kwanza unaitwa Nyumbani ni Nyumbani ambao kwa sasa upo katika hatua ya mwisho na utatambulishwa rasmi wiki ijayo, ni wimbo ambao unazungumzia mambo mbali aliyokutana nayo katika muziki mpaka kuamua kurejea Twanga,” alisema Kalala.
Alisema kuwa ujio wake wa Twanga siyo wa kulazimishwa, bali umetokana na mapenzi yake mwenyewe na hasa akikumbuka fadhira za ASET ambapo ndipo alipata umaarufu mkubwa.
“Nawaomba wadau wa Twanga wakae mkao wa kula, kwani nimerejea kivingine na watarajie kupata mambo mengi mazuri, nitafanya zaidi ya yale niliyoyafanya zamani, lengo ni kuendelea kushika hatamu katika muziki wa dansi,” alisema Kalala ambaye vionjo vyake ‘vimewashika’ mashabiki wengi wa muziki wa dansi.
Afisa Habari wa ASET, Mohamed Pizaro alisema kuwa ujio wa Kalala umetokana na mpango wao waliouanzisha ujulikano Amsha Amsha Twanga Pepeta Nyumbani ni Nyumbani .
Pizaro alisema kuwa mpango huo ni maalum kwa kuhimarisha bendi yao na hasa kwa wanamuziki ambao wameonyesha nidhamu nzuri wakiwa chini ya ASET na sasa wanatumikia bendi nyingine.
Kiongozi msaidizi wa Twanga Pepeta, Saleh Kupaza alimpokea kwa mikono miwili mwimbaji huyo na kusema kazi ya kujihimarisha zaidi imeanza.
“Karibu nyumbani, si unajua nyumbani ni nyumbani, tunaamini hata hao wengine wanajifanya vichwa ngumu, nao watarejea tu,” alisema Kupaza

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.