kiraia kutoa tamko kuhusu Dk Ulimboka

MKUSANYIKO wa Asasi za Kiraia nchini leo unatarajia kuzungumzia suala la kutekwa nyara na kuteswa kwa kiongozi wa madaktari nchini, Dk Stephen Ulimboka aliyerejea nchini kutoka Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa.

Asasi zinazotarajiwa kuzungumzia suala hilo n i Taasisi ya Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Taasisi ya Haki za Raia, Siasa na Mwenendo wa Bunge (CPW), Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), na Chama cha Waandishi wa Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (Misa-Tan).

Mkurugenzi wa CPW, Marcossy Albanie aliliambia gazeti hili juzi kuwa asasi hizo zitazungumza leo, katika Ukumbi wa ofisi za Misa-Tan saa 4.30 asubuhi.

Tutakutana pale katika Ofisi za Misa-Tan siku ya Jumanne (leo) kuzungumzia kitendo cha kupigwa Dk Ulimboka na kufungiwa kwa gazeti la Mwana Halisi.

Undani wa kitakachozungumzwa kuhusu mambo hayo mawili, Watanzania watakijua siku hiyo hiyo,” alisema Albanie.

Ingawa Albanie hakutaka kuweka wazi kitakachozungumzwa kwenye mkutano huo chanzo cha habari kimedokeza kuwa asasi hizo zinatarajia kutoa tamko hilo kuhusu suala hilo la Dk Ulimboka.

Hata hivyo, Jumuiya ya Madaktari hawatakuwepo katika tukio hilo na badala yake watazungumzia suala hilo siku ambayo Dk Ulimboka atazungumza.

Katibu wa Jumuiya hiyo, Edwin Chitage alisema kwamba namna Dk Ulimboka alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari, atazungumza wakati muafaka ukifika.

Kuhusu hali ya kiafya ya daktari huyo, Dk Chitage alisema anaendelea vyema na anapumzika.
Aliwataka Watanzania kuwa na amani kwani Dk Ulimboka atazungumza kwa kina wakati utakapofika.  
Dk Ulimboka alirejea nchini Agosti 12 mwaka huu akitokea Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa baada ya kutekwa na kujeruhiwa vibaya na watu wasiofahamika, kisha kutupwa katika msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Usiku wa kuamkia Juni 26, 2012 watu wasiofahamika walimteka, kumpiga, kumngoa kucha na meno kisha kumtelekeza kwenye msitu huo wa Pande.

Akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), chumba cha wagonjwa mahututi Kitengo cha Mifupa (MOI) alikuwa akihudumiwa na jopo la madaktari zaidi ya saba.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA