KUTOKA KWA MDAU ABDALLAH MRISHO - VODACOM MMEKOSEA KATIKA HILI

Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Vodacom kwa kuja na wazo zuri la kutambua michango na umuhimu wa mitandao ya kijamii, hususan blogs na web site na kuamua kuwatunuku.

Pamoja na pongezi hizo, lakini mmekosea katika utekelezaji wake. Kwa mtizamo wa wahusika wengi (Blogers), tuzo mlizotoa baadhi zimeenda kwa wasiostahili na mmeacha wengi waliostahili kupata tuzo hizo.

Ingawa hamkuweka wazi vigezo vyote, lakini baadhi ya mlivyovitaja ni pamoja na blog kuwa inayofanyakazi (active), ambayo inaweka habari mpya kila siku, iwe inayoandika vitu halisi na siyo vya kukopi au kutafsiri kutoka BBC na mitandao mingine ya Kiingereza na kupesti.

Hali kadhalika mkasema kuwa web site au blog hiyo inachokiandika kiwe kimeandikwa na mtu mwenye ujuzi nacho, mkatoa na mfano kuwa kama ni mapishi, basi yaandikwe na mtu mwenye kujua mapishi. Pia mtandao huo uwe maarufu.

Bila shaka kwenye ulimwengu wa mitandao, unaposema mtandao fulani ni maarufu, ina maana unatembelewa na visitors wengi kwa siku, mtandao hauwezi kuwa maarufu kisha ukawa na visitors 500 au 800 tu kwa siku.

Bloggers maarufu nchini wanajuana na wanahesabika, inakuwa kichekesho inapokuja kutangazwa blog fulani ndiyo maarufu wakati haijulikani hata miongoini mwa bloggers wenyewe, achilia mbali wasomaji wengine.


Hawa ndiyo washindi wenyewe:
  1. Mikocheni Report,
  2. Issa Michuzi
  3. Wanamuziki Tanzania.
  4. Kipanya.co.tz
  5. Vijana FM
  6. Millardayo.com
  7. Taste of Tanzania
  8. Jamii Forums
  9. Mambo Magazine
  10. DJ Fetty Blog
Kwa mtizamo wa wengi, katika orodha hiyo ya watu kumi, ni wanne tu ndiyo walistahili na waliobaki hawakustahili kabisa, kwa sababu licha ya kuwa hawajulikani sana, lakini pia huoni hata namna ambavyo Vodacom, kama kampuni, inaweza kunufaika nao iwapo mtaamua kujitangaza kupitia kwao.

Kuna Bloggers wameachwa ambao wao ku blog ndiyo maisha yao, wanalala, wanaamka, wanatembea, wanakula, wanakunywa, wanakaa wana blog tu. Wao na Blog, Blog na wao. Hakuna taarifa, breaking news au picha za matukio yote muhimu zinazowapita hapa nchini na hata katika kuripoti matukio ya promosheni ya Vodacom kwenye mitandao yao wako mstari wa mbele. Wengine kazi yao ni kukopi na kupesti kazi za wengine!

Pengine hatuyajui malengo ya Vodacom, kwa sababu kama kweli mnanataka kuthamini michango ya 'social media' na wao kunufaika na media hizo, basi mmekosea katika hili.

Waulizeni mliowatuma, wamefanya research ya kutosha na kuona hao washindi wana visitors wangapi na pageviews ngapi kwa siku? Je, Google Analytics Report zao zinaoneshaje? Na, je, habari na picha wanazoziweka kwenye mitandao yao, kweli ni za kwao, au wamekopi na kupesti tu kutoka kwingine?

Naomba mliopewa kazi ya kuandaa tuzo hizi myachukue haya kama changamoto na kuyafanyia kazi ili msiharibu kazi nzuri inayofanywa na Vodacom nchini Tanzania na wala hatuyasemi haya kwa sababu ya chuki binafsi, bali kwa ukweli na uwazi tu!


Wassalaam!

Global Publisherstz.com
"Great achievement, involves great risks"
Abdallah Mrisho
The General Manager
Global Publishers&General Enterprises Ltd
"The House Of Favorite Newspapers"
P. O. Box 7534, Dar es salaam
Tel: +255 22 2773356-7
Mobile: +255 754 290167, 0784 888982
Web Site: www.globalpublisherstz.com
www.abdallahmrisho.blogspot.com

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI