MAHAKAMA YATENGUA UBUNGE WA DK. PETER KAFUMU IGUNGA

 
MAHAKAMA KUU ya Kanda ya Tabora leo imemvua rasmi ubunge, Dk Peter Kafumu, aliyekuwa Mbunge wa Igunga kupitia Tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Hukumu hiyo imetolewa baada ya mlalamikaji Joseph Kashindye aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Tiketi ya Chadema kufungua kesi dhidi ya Peter Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo.
Katika shauri hilo, hoja 15 ziliwasilishwa na wakili wa upande wa mlalamikaji Profesa Abdalla Safari ikiwamo anayodai kwamba Waziri wa Ujenzi John Magufuli alifanya mkutano wa kampeni Kata ya Igulubi wilayani Igunga kutumia madaraka yake kuahidi ujenzi wa Daraja la Mbutu kama wananchi hao watampigia kura mgombea wa chama mapinduzi.
Pia Safari anadai waziri huyo aliwatisha wananchi wa kata hiyo kwamba wasipo ichagua CCM daraja hilo halitajengwa na kwamba pia aliwatisha wananchi hao kuwa wasipomchagua Dk Kafumu watashughulikiwa.

Profesa Safari alidai Baraza la Waislamu (Bakwata) Wilaya ya Igunga liliwakataza waumini wasiipigie kura Chadema na kwamba naye Rais mstaafu, Benjamini Mkapa alitoa ahadi ya kugawa mahindi kwa wananchi wa Igunga siku moja kabla uchaguzi ili waichague CCM.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI