''Marekani haikuhusika na mauaji ya mhubiri''


Vurugu Mombasa

Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi umekanusha madai ya kuhusika na mauaji ya kiongozi mmoja wa kidini mjini Mombasa, Sheikh Aboud Rogo.

Wakili wa Rogo, Mbugua Mureithi na viongozi wengine wa Kiislamu wamedai kuwa Marekani ilihusika na mauaji ya kiongozi huyo wa kidini aliyepigwa risasi na watu wasiojulikana mjini Mombasa.

Makanisa kadhaa yaliteketezwa na makundi ya vijana waliokuwa wakipinga mauaji hayo.
Lakini ubalozi huo umesema madai hayo hayana msingi wowote.

Hali imetulia mjini Mombasa baada ya usiku wa makabiliano mapya mjini humo kufuatia shambulizi la guruneti ambapo mtu mmoja aliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Shambulio hilo limefuatia muda wa utulivu baada ya siku mbili ya makabiliano makali kati ya vijana waliofanya maandamano na polisi ambapo maafisa wanne wa polisi waliuawa.

Ghasia hizo zilisababishwa na kuuawa kwa mhubiri wa kiislamu Aboud Rogo Mohammed,aliyetuhumiwa na umoja wa mataifa pamoja na Marekani kuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi

Mkuu wa polisi katika mkoa wa pwani ni Aggrey Adoli ameithibitishia BBC tukio hilo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA