MBARONI KWA KUHAMASISHA WANANCHI WASUSIE ZOEZI LA SENSA TANGA

 TANGA, TANZANIA
Wakati siku zikikaribia za kufanyika zoezi la Sensa ya watu na makazi, Mratibu mmoja wa Elimu Kata ya Vugiri wilayani Korogwe, Tanga, Juma Salehe (52) amekamatwa na polisi akihamasisha mitaani kwa kipaza sauti wananchi walikatae zoezi hilo.

Habari zilizofikia meza ya  CCM Blog,  zimesema mratibu huyo wa elimu ambaye anadaiwa kuwa pia ni Sheikhe wa Msikiti wa Mazinde katika kata hiyo ya Vugiri anashikiliwa katika kituo cha mamlaka mji mdogo wa Mombo uliopo wilani ya Korogwe vijijini mkaoni Tanga.

Imeelezwa amekamatwa jana saa 8.00 mchana ndani ya msikiti wa Mazinde, kutokana na  wananchi kutoa taarifa dhidi ya mtu huyo kuendesha vitendo ambavyo vilikuwa vikiwachanganya wananchi kuhusu zoezi hilo la Sensa.

"Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa maandalizi ya shitaka lake", amesema Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,Coastantin Massa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA