MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WAWAPIGA MSASA WAHARIRI WASANIFU NA WATAYARISHAJI VIPINDI

 Baadhi ya viongozi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, wakiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Kituo cha Maendeleo cha Wahariri Wasanifu na Watayarishaji Vipindi Tanzania (KIMAWATA), wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuwezesha wanachama wa kituo hicho kuhusu shughuli za mfuko ili waweze kuandaa habari wanazoletewa vema/vizuri. Warsha hiyo ya siku moja  inafanyika leo kwenye Hoteli ya Nashera, mjini Morogoro.
 Wanachama wa KIMAWATA wakijadiliana mambo baada ya kutoka kupiga picha ya pamoja
Wanachama wa KIMAWATA wakiingia ndani ya ukumbi wa Hoteli ya Nashera kuendelea na warsha
Meneja wa Mfuko wa LAPF, Andew Ruubyana (katikati), akizungumza na Meneja Uwekezaji wa mfuko huo, Elias Baruti (kushoto) pamoja na Rehema Mkamba ambaye ni Ofisa Uhusiao wa LAPF.

 Meneja Uhusiano wa Mfuko wa LAPF, Andrew Ruubyana akitoa muhtasari wa ratiba ya warsha hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa KIMAWATA, Lauden Mwambona.
Sehemu ya wahariri wasanifu na watarajishaji vipindi wakiwa makini kuandika taarifa muhimu wakati Meneja wa Kanda ya Masharki wa mfuko huo, Sayi Lulyalya (hayupo pichani)
 Charles Chacha (kushoto) wa The Citizen akiwa na Amana Nyembo (katikati) wa Tanzania Daima pamoja na Anitha Challi wa Radio Times wakiandika mambo muhimu.
 Mwenyekiti wa KIMAWATA, Laudeni Mwambona akielezea uhuhimu wa wanachama wake kuujua mfuko huo. Kutoka kulia ni Sayi Lulyalya Meneja wa Kanda ya Mashari wa Mfuko huo na Andrew Ruubyana ambaye ni Meneja Uhusiano wa LAPF.
 Wanachama wa KIMAWATA, Hamida Shariff  (kushoto) wa Mwananchi Morogoro na Stephen Baligeyo wa Uhuru (katikati) wakiwa kwenye warsha hiyo
Katibu wa KIMAWATA, Boniface Luhanga (kushoto) na  Jane Mathias ambaye ni Mhariri Msanifu wa gazeti la Nipashe wakifuatilia kwa makini katika warsha hiyo
 Wanachama wa KIMAWATA, wakifuatilia moja ya mijadala iliyokuwa inaendeshwa katika warsha hiyo. Kutoka kushoto ni Jane Mathias wa Nipashe, Ally Mkoreha wa Mwananchi, John Stephen wa Mwananchi na Pius Ntiga wa Radio Uhuru.
 Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwessa (kushoto) na Grace Semfuko wa Star Televisheni wakifuatilia mambo muhimu wakati wa warsha hiyo.
 Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Sayi Lulyalya akielezea khuhusu utendaji na manufaa ya kujiunga na mfuko huo.
Wanachama wa KIMAWATA kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kwenye semina hiyo ya kupigwa msasa

 Sayi wa LAPF (katikati) akiendelea kuwapiga msasa wanachama wa KIMAWATA
 Mmiliki wa Blogu ya Full Shangwe, John Bukuku (kulia) akishiriki kwenye semina hiyo kwa lengo la kuuelewa mfuko huyo pamoja na kurusha habari za warsha hiyo kwenye Blogu.
Mwenyekiti wa KIMAWATA, Laudeni Mwambona (aliyevaa tai) akizungumza na  Jane Mihanji wa gazeti la Uhuru pamoja na Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, Anicetus Mwessa (PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU