MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AZINDUA SHULE YA SEKONDARI MAENDELEO HUKO NAKASANGWE MADALE JIJINI DAR ES SALAAM


 Mwenyekiti wa Kia motors, Cho Kwi Hyun akikabidhi Kuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik mfano wa ufunguo wa moja ya magari manne ambayo kampuni hiyo imetoa kwa shule ya Maendeleo iliyopo  Nakasangwe Madale wakati wa hafla ya uzinduzi wa shule hiyo leo kulia ni Mkurugenzi Shirika (GNI), Yang Jin OK na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali Mtaa Madale Alex Mbuya
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik akihutubia wananchi wakati wa uzinduzi wa shule ya Maendeleo iliyoko Nakasangwe Madale jijini Dar es salaam iliyojengwa  kwa msaada wa kampuni ya  KIA na HYUNDAI za Korea kupitia shirika la Good Neighbor International la Korea
Vijana mbalimbali kutoka Shirika la GNI nchini Korea walioshiriki kujitolea kujenga shule ya Sekondari Maendeleo Nakasangwe huko Madale  wakiwa katika hafla ya uzinduzi leo.


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaaam Said Mecky Sadik ameitaka Manispaa Kinondoni inahakikisha kuwa wanakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 249 kwa ajili ya watotoa watakaofaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka ujao.
 Kauli hiyo aliitoa leo, wakati wa uzinduzi wa shule ya sekondari Maendeleo, iliyojengwa kwa msaada wa Shirika la Good Neighbor (GNI), kwa kushirikiana na Kia Motors kutoka Jamhuri ya Korea.
 Sadik alisema ujenzi wa vyumba hivyo utasaidia kuwafanya watoto zaidi 18000 wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza katika wilaya hiyo kuanza masomo kwa wakati.
 Aliwataka viongozi wa Wilaya hiyo, kutekeleza kwa vitendo ahadi waliyotoa kuwa ifikapo mwishoni mwa  Desemba mwaka huu watakuwa mmekamilisha ujenzi wa vyumba hivyo.
Akizungumzia kuhusu shule hiyo, Sadik alisema ujenzi wa shule hiyo utasaidia katika kuwapatia watoto elimu bora.
 “Mmepata msaada huu lakini ni washauri kuwa unapobebwa ni lazima ujikaze hivyo msibweteke bali mhakikishe mnazilinda mali za shule hii kwa nguvu zenu zote”alisema Sadik.
 Vilevile alisema uwezekano wa mtaa huo kupatiwa nishati ya umeme inawezekana, lakini bado wakazi wa maeneo waache kujenga bila kufuata taratibu za mipango miji kwa ajili ya huduma za jamii.
 Naye Mwenyekiti wa Kia motors, Cho Kwi Hyun alisema ukiachilia mbali ya ujenzi wa shule hiyo, pia wamekabidhi magari manne yatakayotumika kusafirisha wanafunzi na huduma nyingine za kijamii katika mtaa huuo.
 Kwa Upande Mkurugenzi Shirika (GNI), Yang Jin OK alisema mradi huo utakuwa wa miaka mitano hivyo anawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa ajili ya kujisogezea

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA