Mratibu wa Tamasha la Injili la Pasaka Tanzania, Alex Msama (kushoto), akimkabidhi msaada wa sh. mil. 1, mchezaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Alphonce Modest za kusaidia matibabu ya miguu inayosumbuliwa na baridi yabisi. Msaada huo uliokabidhiwa Dar es Salaam leo, ulihamasishwa na Mhariri Kiongozi wa gazeti la Champion, Saleh Ali (wa pili kushoto) pamoja na Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten na Radio Magic FM, Said Kilumanga (wa pili kulia). Wameiomba Jamii yenye huruma kumsaidia kwa hali na mali mchezaji huyo ambaye wamemsafirisha kwa gharama zao kutoka Mwanza. (PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)
|
Modest akitembea kwa taabu huku akisaidiwa na mdogo wake Francis |
|
Jinsi alivyo kwa sasa Modest |
Alex Msama akielezea jinsi alivyoguswa kumsaidia Modest na kutoa mwito kwa watanzania kumuunga mkono kwa kumsaidia mchezaji huyo wa zamani ambaye anahitaji fedha za kumtibia katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)
|
Modest akitoa shukrani kwa Msama na kuelezea jinsi ugonjwa huo ulivyompata na kumsababishia kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza kwa mwaka mzima wa 2011 |
Kilumanga ambaye ni mmoja wa wahamasishaji waliowezesha kupatikana msaada huo kutoka kwa Msama, akiendelea kuuhamasisha umma kmsaidia kwa hali na mali Modest apate kupona.
Saleh Ali ambaye pia ni mmoja wa wahamasishaji, akiwaomba wasamaria wema kuendelea kumsaidia Modesti kwa hali na mali.
Comments