MUNGAI NA MWAKALEBELA HAWATAFUTWI NA TAKUKURU - WAKILI

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Edward Hosea.SAKATA la taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa kuendelea kuwang'ang'ania wanasiasa Joseph Mungai na Frederick Mwakalebela limechukua sura mpya baada ya wakili wa wanasiasa hao kuitaka TAKUKURU kuwasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali kabla ya kupotosha umma.

Akizungumza na waandishi wa habari jana wakili wa Mungai na Mwakalebela Basil Mkwata alisema kuwa katika taarifa ya TAKUKURU kwa vyombo vya habari juzi imeonyesha kuwa Fredrick Mwakalebela kafunguliwa mashitaka upya.

“Napenda kuufahamisha umma kupitia kwenu ya kwamba
sheria inampa mtu asiyeridhika na uamuzi wa mahakama kuu kukata rufaa kwenda mahakama ya rufaa”

Alisema kuwa Kanuni ya 68(1) ya Kanuni za Mahakama Rufaa za 2009 inasema kwamba mtu anayetaka kukata rufaa kwenda mahakama ya rufaa atafanya hivyo ndani ya muda wa siku thelathini kuanzia tarehe ya uamuzi kwa kutoa notisi kwenda mahakama kuu husika.

Kwa mujibu wa kanuni hiyo notisi hiyo ndiyo hufungua rufaa. Mzee Mungai na Mwakalebela tayari wamekwisha tumia haki yao hiyo kwa kupeleka notisi zao za rufaa na rufaa zao kufunguliwa kama na. 13 na 14. Kwahiyo taarifa ya Takukuru inakinzana na ukweli huu.

“Tatizo ninaloliona hapa ni aidha huyo kamanda wa Takukuru kutokujua tafsiri ya Kanuni niliyoitaja kwamba ni wakati gani rufaa huchukuliwa kuwa imefunguliwa katika Mahakama ya rufaa au ni kutokuwepo na mawasiliano baina ya ofisi yake na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndiye mhusika wa kesi hiyo katika ngazi ya Mahakama Kuu au ni tatizo la kutaka kujitafutia umaarufu kama tulivyozoea kuona”

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA