BALOZI MAHALU ASHINDA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

 Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu (kulia), akikumbatiana kwa furaha na mmoja wa ndugu zake baada ya kushinda kesi yake katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo, wakati wa kutolewa hukumu wa kesi yake ya kuhujumu uchumi na kusababishia hasara Serikali ya Euro milioni 2 wakati akiwa balozi nchini humo. Profesa Mahalu ameshinda katika hukumu iliyotolewa na Mahakama hiyo.
                          Mahalu akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuachiwa huru
 Mmoja wa washitakiwa aliyeshitakiwa pamoja na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, Grace Martine (katikati), akisaidiwa na ndugu zake kutoka Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo, baada ya kushinda kesi yao ya kuhujumu uchumi na kuisababishia hasara Serikali ya jumla ya Euro milioni 2.
Wakili wa kesi ya Mahalu,  Mabere Marando, akizungumza na vyombo vya habari baada ya hukumu hiyo

Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Italia, Prof.Costa Ricky Mahalu (63), ameachiwa huru mchana huu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo baada ya kuonekana kuwa hana hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili yeye na Afisa ubalozi Grace Martin, ya kuisababishia serikali hasara ya euro 2,065,827.60.
 
Akitoa hukumu yake, Hakimu Mkazi Mfawidhi Illivin Mgeta amesema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kutoa ushahidi wa kutosha kiasi cha kuwatia hatiani washtakiwa Mahalu na Grace.
Awali, hukumu ya kesi hiyo iliahirishwa mwezi uliopita na Hakimu Katemana, kwa maelezo kuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mgeta aliyekuwa akiisikiliza kesi hiyo kukosekana kwavile alikuwa akikabiliwa na majukumu mengine.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na mawakili waandamizi wa serikali, Ponsiano Lukosi, Vincent Haule na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Linkolin, uliita mashahidi saba na vielelezo tisa vikiwemo mikataba miwili ya ununuzi wa jengo la ubalozi jijini Rome, Italia na upande wa utetezi uliita mashahidi watatu, akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA