Rais Kikwete amlilia Kapteni (mst) James Charles Yamungu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa John Gabriel Tupa salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Kepteni (mst) James Charles Yamungu kilichotokea alfajiri ya leo, Jumatano, Agosti 22, 2012, kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.

Katika salamu hizo, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Tupa, “ Nimepokea kwa huzuni na mshtuko taarifa za kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Kepteni Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Mheshimiwa James Yamungu. “

Amesema Rais Kikwete katika salamu hizo: “ Kifo cha Kepteni Yamungu kimeinyang’anya nchi yetu na Serikali yetu mtumishi hodari na mwadilifu wa umma ambaye katika utumishi wake wote tokea alipokuwa Jeshi hadi anaingia uongozi wa siasa alithibitisha uaminifu wake kwa nchi yetu na uongozi wake.”

“Kufuatia msiba huu mkubwa, nakutumia wewe Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Tupa,  salamu zangu za rambirambi, na kupitia kwako naitumia salamu zangu za dhati kabisa familia ya marehemu, wana-Mara na Wana-Serengeti wote ambako ndio kwanza alikuwa ameripoti kuanza kazi yake ya ukuu wa wilaya hiyo,” amesema Mheshimiwa Rais Kikwete na kuongeza:

“Napenda kuwajulisheni kuwa moyo wangu uko nanyi katika kipindi hiki kigumu. Nawaombea uvumilivu na subira na naungana nanyi kumwomba Mwenyezi Mungu,  Mwingi wa Rehema, aiweke pema peponi roho ya Marehemu James Charles Yamungu. Amen.”


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
22 Agosti, 2012

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI