Sakata la uvunjaji wa nyumba, vibanda vya wavamizi Madale, Dar es Salaam
Baadhi ya wakazi wa eneo la wazi lililovamiwa na kumilikiwa isivyo halali na watu maeneo ya Madale, Kinondoni Dar es Salaam, ambako Polisi walikuwa wakiendesha oparesheni ya kuvunja nyumba na vibanda vyao, wakiwa wamewekwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Askari Polisi akiangalia mabaki ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya kinondoni wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Askari Polisi akiangalia badhi ya vifaa vilivyokuwemo ndani ya moja ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Askari Polisi wakiangalia mabaki ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

Askari Polisi, akimuongoza mmoja wa vijana waliokuwa wakiwatishia, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi maeneo ya wazi, Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam kuelekea kwenye gari tayari kwa kuwapeleka kituoni leo.

Mmoja wa askari Polisi, akimuongoza kijana mwingine aliyekuwa akiwatishia, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi maeneo ya wazi, Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam kuelekea kwenye gari tayari kwa kuwapeleka kituoni leo.

Askari Polisi wakiwa wamesimama sehemu kilipobomolewa moja ya vibanda leo, vilivyojengwa kwenye sehemu za wazi zinazodaiwa kuvamiwa isivyo halali na watu ambao walikuwa wakiviuza kwa baadhi ya wananchi maeneo ya Madale, Kinondoni, Dar es Salaam.
Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likivunja moja ya vibanda vilivyojengwa kwenye eneo lililovamiwa maeneo ya Madale Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

Dereva wa gari la Jambo Leo, Privatus Kachema, akiangalia zoezi la uvunjaji wa nyumba na vibanda vya wavamizi maeneo ya Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo.


Moja ya nyumba zilizovunjwa katika oparesheni ya uvunjaji wa nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi la Madale leo.

Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likivunja moja ya vibanda vilivyojengwa kwenye eneo hilo la wazi.
Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likiendelea kuvunja moja ya vibanda vilivyojengwa kwenye eneo.
Askari Polisi na Mgambo wa Manispaa ya Kinondoni, wakikagua moja ya kibanda kabla ya kuvunjwa na tingatinga la Manispaa hiyo, wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo.
Askari Polisi na mgambo wa Manispaa ya Kinondoni wakiangalia tingatinga la Manispaa hiyo, wakati likivunja nyumba na vibanda vilivyojengwa kwenye sehemu za wazi zinazodaiwa kuvamiwa isivyo halali na watu ambao walikuwa wakiviuza kwa baadhi ya wananchi wengine maeneo ya Madale wilayani humo.


Askari Polisi wakiangalia mabaki ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.



Moja ya bango lililokutwa limeandikwa na watu hao, likiwa na ujumbe uliokuwa ukimshutumu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela na OCD wake.


Mmoja wa watu wanaodaiwa kuwa wavamizi wa eneo hilo, aliyejitambulisha kwa jina la Hussein Said, akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kupata athari kichwani wakati alipokuwa akiwekwa chini ya ulinzi na askari Polisi kwenye maeneo hayo. Chanzo. Bayana Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*