SIMBA YAWATEMA MBIVAYANGA, MRWANDA YASAJILI BEKI MKENYA NA STRIKER LA IVORY COAST

Paschal Ochieng

Kwa hisani ya Mahmoud Zubeiry wa Bin Zubeiry Blog
SIMBA SC imevunja mkataba na kiungo Kanu Mbivayanga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na mshambuliaji mzalendo Danny Mrwanda na kusajili wachezaji wawili wengine wa kigeni, beki Paschal Ochieng na mshambuliaji Daniel Akuffo kutoka Ivory Coast.
Mshambuliaji kutoka Ivory Coast tayari yupo Dar es Salaam tangu saa 3:00 asubuhi na jioni ya leo atakwenda kuungana na kikosi cha Simba kilichopo kambini Arusha, wakati Ochieng kutoka AFC Leopard ya Kenya tayari mtu amekwenda kumpokea mpakani, Namanga.
Kwa maana hiyo, Simba sasa inakuwa na wachezaji wa kigeni watano, baada ya Waganda Emmanuel Okwi, Mussa Mudde na Mzambia Felix Sunzu.
Habari za ndani kutoka Simba SC, ambazo zimeifikia BIN ZUBEIRY zimesema kwamba marekebisho hayo ya usajili yanatokana na ushauri wa Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Profesa Milovan Cirkovick, raia wa Serbia.
Cirkovck ameamua kumuondoa kwenye kikosi chake Mrwanda, kwa sababu amempata Mrisho Ngassa na Kanu ametemwa kwa sababu timu ina viungo wengi, hivyo ameona bora kuongeza beki mmoja na mshambuliaji.
Wakati huo huo, kiungo Kiggi Makassy aliyesajiliwa kutoka Yanga, sasa anahamishiwa kwenye nafasi ya beki ya kushoto akagombee namba na Amir Maftah na Paul Ngalema.
Beki wa kulia, Haruna Shamte ana asilimia sawa za kubaki au kutemwa kwenye kikosi cha Simba, kwani Cirkovick anaona bora kuwatumia wachezaji wa Simba B, ambao wanafanya vizuri na wapo hadi timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes.
Katika beki ya kati, baada ya kumpata Ochieng, Milovan anaamini akiungana na Juma
Nyosso, Shomary Kapombe na Obadia Mungusa atakuwa ana ukuta umara.
Lakini Milovan anataka kuangalia hali ya timu hadi Desemba na kama ataona kuna haja ya kurekebisha tena kikosi kabla ya kuingia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, atafanya hivyo.
Mrwanda alisajiliwa Simba kwa ajili ya msimu ujao, akitokea Vietnam alipokuwa akicheza soka ya kulipwa sawa na Kanu aliyesajiliwa kutoka DRC. Wakati Mrwanda anasajiliwa Simba, na Yanga pia walikuwa wanamtaka, lakini Wekundu wa Msimbazi wakawazidi dau wapinzani wao wa jadi.
Aidha, Simba inamsajili Ochieng kuchukuan nafasi ya Mbuyu Twite kutoka APR, ambaye alisaini kwa Wekundu hao wa Msimbazi, baadaye akaghairi na kwenda Yanga.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.