TANZANIA YAANZA KWA SARE AIRTEL RISING STAR AFRICA

Kikosi cha Tanznaia cha Airtel Rising Star kilichotoa sare jana

Na Princess Asia
TIMU ya taifa ya Tanzania ya Airtel Rising Stars jana imetoka sare ya bao 1-1 na Burkina Fasso, katika michuano ya Airtel Rising Star Afrika, Uwanja wa Nyayo, mjini Nairobi, Kenya.
Matokeo hayo yanaiweka Tanzania shakani kusonga mbele katika michuano hiyo baada ya jana kuianza vibaya kwa kukubali kufungwa bao 1-0 na Gabon katika mchezo wake wa kwanza.
Kufuatia matokeo hayo Tanzania inasubiri bahati tu ili kusonga mbele kwani sasa itabidi kushinda mchezo wake wa mwisho utakaofanyika kesho 23/08/2012 dhidi ya Zambia na wakati huo huo kuiombea Gabon iifungwe na Zambia katika mchezo wao wa mwisho. Kila kundi itatoa timu moja kusonga mbele hatua ya robo fainali zinazotarajiwa kuanza kesho kutwa.
Katika mchezo wa jana, Burkina Fasso ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kushtukiza katika dakika ya kwanza ya kipindi cha pili na hivyo kuwafanya vijana hao wa Tanzania kutulia na kuanza kucheza pasi za kuonana hali iliyozaa matunda dakika kumi baadaye.
Goli la kusawazisha la Tanzania lilipachikwa kimiani na mshambuliaji wake hatari Paulo Balama aliyepokea pasi akiwa kati ya uwanja na kuchanja mbuga kuelekea langoni mwa wapinzani wao, ambapo kabla ya kufunga aliwapunguza mabeki watatu na kisha kumlamba chenga kipa wa Burkina Fasso na kuachia kiki kali iliyokwenda moja kwa moja wavuni.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Kocha na mkuu wa msafara wa timu
ya Tanzania, Salum Madadi alisema vijana wake walicheza vizuri isipokuwa tatizo ni kutopata muda wa kutosha wa wachezaji wake kuzoeana hasa ikizingatiwa kuwa timu hiyo inaundwa na kombaini ya wachezaji kutoka mikoa sita tofauti.
"Kwa mfano mchezo wetu wa juzi dhidi ya Gabon vijana walicheza vizuri sana pamoja na tatizo la kutozoeana hata hivyo waliweza kuwabana wapinzani kwa muda mwingi na hata kufika langoni mwa wapinzani wetu kwa kupiga mashuti kadhaa ila bahati haikua yetu tu," alisema Madadi.
Matokeo mengine ya mechi zilizochezwa jana kwa wanaume ni Kenya kutoka sare ya 1-1 na Ghana, Malawi pia kutoka sare ya 1-1 na Madagascar, Nigeria kutoka sare ya 1-1 na Niger, Congo DRC kuichakaza Chad bao 5-0 na Zambia kuichapa Burkina Fasso 5-0. Kwa upande wa wanawake Congo DRC iliichakaza Burkina Fasso magoli 8-0, Ghana nayo ikaichapa Kenya bao 7-2, Chad ikaifunga Nigeria bao 1-0 na Uganda kuifunga Sierre Leone
3-0.
Michuano hiyo ya Airtel Rising Stars kwa ngazi ya Afrika iliyoanzishwa kwa lengo la kuibua vipaji kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, Inafikia kilele keshokutwa kwa bingwa kupatikana ambapo mshindi huyo atapata nafasi kwa wachezaji wa timu nzima kuhudhuria kliniki ya soka ya kimataifa itakayoendeshwa na jopo la makocha kutoka klabu ya Manchester United na Arsenal za Uingereza itakayofanyika kuanzia Agosti 26 hadi 30 mwaka huu jijini Nairobi.Chanzo; Bin Zubeiry Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.