Taswira Mbalimbali Za Mikutano ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Godbless Lema

 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia ni  Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwasili kwenye  Uwanja wa Kwa Mbombe katika kijiji cha Madizini, Kata ya Mtibwa mkoani  Morogoro ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Opereshi Sangara juzi.
 Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kabla ya Mahakama kutengua Ubunge wake, Mh Godbless Lema amefungua matawi katika Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha juzi August 18,2012.
Katika ziara hiyo, Lema aliambatana na Mbunge wa Arumeru Masariki Mh Joshua Nassari(wa pili kulia) pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM kabla ya kujiengua na kujiunga na Chadema mapema mwezi Aprili mwaka huu, Ndg James Ole Millya, ambao nao kwa nyakati tofauti walipata fursa ya kuzunumza.
 
Mbali na suala la uzinduzi na upokeaji wanachama wapya, Lema alifanya harambee ya kukusanya fedha kusaidia shughuli za chama hicho katika Kata hiyo ambapo jumla ya Sh 219,500 zilichangwa na wananchi.
 
Akiondoka eneo hilo, Lema alilazimika kuwatuliza mamia ya watu waliokuwa wanafuatilia msafara wake ili kuepusha kutokea mwanya kwa watu wenye nia mbaya kuleta vurugu na uharibifu wa mali. Baadae msafara wake  ulikatiza mitaa ya Stand Kuu ya mabasi makubwa na kisha kuelekea bustani ya City Park huku njiani akishangiliwa sana na baadhi ya watu wakinyoosha vidole  kama ishara ya ushindi.
 Wanachama wapya aliojiunga na chadema wakigombania kadi za chama hicho
 Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kabla ya Mahakama kutengua Ubunge wake, Mh Godbless Lema akiunguruma kwenye uzindusi wa  matawi katika Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha juzi August 18,2012.
Jitihada za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) za kuwafikia  wanachi ili kunadi sera zake, hususan katika mikutano inayoendelea katika mkoa wa Morogoro, zilikumbana na vikwazo mbali mbali katika baadhi ya maeneo, kama inavyoonyesha pichani, mtaro uliochimbwa katika barabara ya  kuingia kijiji cha Namgezi kitongoji cha Kambi ya Keya jimbo la Ulanga  Mashariki, kwa lengo la kuzuia magari yasipite.Picha na Joseph Senga

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI