Timu za Tanzania za Kikapu zaenda Uganda Zone Five

Makamu wa Rais - TBF Phares Magesa mwenye fulna nyeupe katikati akizungumza na kuwaaaga wachezaji hao wengine kutoka kushoto Father Swai Mkurugezi wa Don Bosco, Kanali Busungu Mkurugenzi wa Michezo JWTZ, Msoffe Katibu Mkuu TBF, Father Marco don Bosco,na Meja Budodi Mkuu wa Msafara na Kamisha wa wanawake TBF.

Wachezaji na  Viongozi wa timu zote, TBF , Don Bosco na JWTZ. 
********************
Timu 4 za Tanzania za Kikapu zimeondoka leo kwenda Kampala, Uganda kushiriki mashindano ya kutafuta bingwa wa kikapu wa kanda ya tano ya Shirikisho la mpira wa kikapu Duniani - FIBA ( FIBA zone 5 Club Championship).

Timu zetu zinazoshiri mashindano hayo ni Savio kutoka Don Bosco ambao ndio Mabingwa wa Tanzania upande wa wanaume na washindi wa pili ABC, na kwa upande wa wanawake ni Jeshi Stars ambao ndio mabingwa wa Tanzania na washindi wa pili ni Don Bosco Lioness.

Kila timu imeondoka na wachezaji 12 na viongozi watatu, mkuu wa msafara ni Kamishna wa wanawake katika TBF, Meja Specioza Budodi (Mrs.), viongozi wengine wa juu wa TBF watakwenda Kampala baade akiwemo Ndg. Alexander Msoffe ambaye ni mjumbe wa bodi ya FIBA kanda ya 5.

Msafara huo uliagwa rasmi na Makamu wa Rais wa TBF ndg. Phares Magesa katika viwanja vya ABC - Chang'ombe leo asubuhi, pia walikuwepo Kanali Busungu ambye ni Mkurugenzi wa Michezo katika JWTZ, Katibu Mkuu wa TBF ndg. Alexander Msoffe na Mkurugenzi wa kituo cha Don Bosco Father Swai.

Kwa sasa bingwa kikapu kanda ya 5 ni timu ya Urunani toka Bunjumbura, Burundi kwa upande wa wanaume na Kenya Ports Authority(KPA) toka Mombasa , Kenya ambao walichukua ubingwa katika mashindano yaliyofanyika Dar es Salaam mwaka jana. Mshindano haya yanashikisha timu 2 za wanaume na wanawake washindi wa juu kutoka katika kila nchi za kanda hii ya 5 inayojumuisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Somalia, Sudani, Sudani ya Kusini, Eritrea na Misri.

Pia mashindano ya kanda ya 5 kwa timu za Taifa mwaka huu yatafanyika Dar Es Salaam Tanzania mwezi desemba, hivyo ushiriki wa timu zetu 4 katika mashindano ya vilabu huko Kampala yatasaidia kuwanoa wachezaji wetu na ni matumani yetu watafanya vizuri na baadae wale watakochaguliwa katika timu zetu za taifa basi pia watatuwakilisha vizuri.

Tunawashukuru sana Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Precision Air na wafadhili wengine walisaidia kufanikisha safari hii na kuwezesha kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu Tanzania kupeleka nje timu 4 katika mashindano haya.

Tunaomba wafadhili wengine waendelee kujitokeza kusaidia michezo na hususani mchezo wa kikapu ili kufanikisha malengo yetu na kutumiza wajibu wetu katika jamii yetu.

Tunawatakia kila la heri na tuwaombee Mungu wafanye vizuri katika mashindano haya na kuitangaza vizuri nchi yetu.

Imetolewa na:
Phares Magesa,
Makamu wa Rais- TBF
0784/0767/0713 618320

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI