Uganda yavuna medali ya dhahabu

Steven Kiprotich (pichani) wa Uganda amekishangaza kikosi kikali cha Wakenya na kushinda mbio za marathon kunako siku ya kuhitimisha michezo ya Olimpiki ya London 2012.

Medali hii ya dhahabu kwenye mashindano ya mwaka huu ni ya pili kwa Uganda tangu mwaka 1972 marehemu John Akii Bua aliposhinda mbio za mita 400 kuruka viunzi kwenye mashindano ya Munich.

Kiprotich ameshinda mbio hizi katika mda wa saa 2 dakika 08 na sekunde 01 kupitia mitaa ya jiji la London akiwa mbele ya mshindi wa mara mbili wa mbio za marathon na bingwa mtetezi Abel Kirui aliyemaliza wa pili katika mda wa saa 2 dakika 08 na sekunde 27.

Mkenya mwingine aliyeongoza mbio za leo kwa kipindi kirefu Wilson Kipsang, ameshinda medali ya shaba akimaliza katika mda wa saa 2:09.37.

Kiprotich, Kiprotich na Kirui

Hii ni medali ya pili ya dhahabu kwa Uganda kwenye mashindano ya Olimpiki baada ya miaka 40. Medali nyingine ya mashindano ya Olimpiki ilikua ya fedha mkimbiaji wa mbio za mita 400 Davis Kamoga alipofukuzana na bingwa wa nyakati hizo Michael Johnson wa Marekani mwaka 1996.

Mbio hizi kwa kipindi cha kilomita 10 kilitawaliwa na Franck De Almeida kutoka Brazil ikiashiria mbio kali zitakazowaniwa kati ya Wakenya na Waethiopia. Lakini mbinu za Ethiopia zilichachuka pale Dino Sefir alipoonekana kuishiwa nguvu na kasi yake kupungua na Kipsang kuanza kuwasha moto na kuongoza kupitia mitaa kadhaa ya Jiji.

Mkenya huyu aliweka pengo la sekunde 30 kupitia eneo ambalo lina vivutio safi vya mji wa London na kufikia kituo cha kilomita 30 mwanariadha wa pili wa Ethiopia Getu Feleke akaonyesha dalili za kukata tamaa na kuonekana kurudi nyuma.

Kufikia eneo lilikua na watazamaji wengi sana Kiprotich akaongezea mafuta miguu na kuanza kumkimbiza Kipsang akigawanya kikundi cha wakimbiaji waliokua wakisaka nafasi nono za medali.

Hatua yake ilisababisha kuwaamsha Wakenya, kwanza mshindi wa Marathon za Dubai Ayele Abshero wa Ethiopia aliyepunguza pengo lililowekwa na Kipsang hadi sekunde 11 na kufikia kilomita 25 walikua pamoja.

Watazamaji wa mashindano ya Olimpiki

Hadi kilomita 30 Abshero alianza kuona mwendo kua na uchungu na miguu mizito na kuachwa nyuma kwa sekunde 36 na hata kupitwa na Marilson Dos Santos wa Brazil.

Kundi lililokua likiongoza kupitia sehemu iliyofunikwa ya soko la Leadenhall kuingia hatua ya kilomita saba za mwisho, Wakenya walijitahidi kumuacha Kiprotich.

Lakini Kiprotich akiwaonelea wa Kenya walio mbele yake wakisinzia na kuweka kasi yake juu na kuwapita kwenye hatua ya kilomita 32 na kuwashangaza alipowaacha kwa tofauti ya mita 200.

Kiprotich, ambaye alihamisha mazowezi yake katika eneo maarufu la mazowezi huko Eldoret ambako amejiunga na bingwa wa zamani wa mbio za mita 5000 Eliud Kipchoge, aliongezea kasi yake na kudhibiti nafasi yake mbele.

Kupitia kilomita mbili za mwisho, Mganda huyo mwenye umri wa miaka 23 alikua mbele ya Kirui kwa tofauti ya sekunde 20 na aliweza kupata mda wa kuchungulia anayemfuta yuko wapi kabla ya kunyakua bendera ya Uganda kwenye hatua yake ya mwisho akiingia Mall, pembezuni mwa Kasri ya Buckingham, na kuivaa shingoni wakati akivuka mstari wa kumalizia mbio hizi.
Kumaliza mbio
1 Kiprotich UGA 2:08:01 - Dhahabu
2 Kirui KEN 2:08:27 - Fedha
3 Kiprotich KEN 2:09:37 - Shaba

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*