USAJILI WA PASCAL OCHIENG WAZUA UTATA SIMBA


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zakaria Hanspope akimkabidhi jezi namba 5 mchezaji mpya wa klabu hiyo,Pascal Ochieng. Katikati ni Makamu Mwenekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu'

NAIROBI, Kenya
MATARAJIO ya Wekundu wa Msimbazi kupata huduma za beki wa zamani timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars,’ Pascal Ochieng, yako shakani baada ya klabu ya AFC Leopards kudai ni mchezaji wao halali.


Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la nchini humo, Katibu Mkuu wa Leopards, ambayo ni klabu ya zamani ya Ochieng, Winstone Kitui, amesema klabu yake imesikitishwa kusikia kuwa nyota huyo amesaini mkataba wa miaka miwili Simba.


Aliongeza kuwa, wameshitushwa kusikia usajili huo wa mabingwa wa Tanzania Simba kwa beki wao huyo, aliyejifunga kwa mkataba mfupi wa kuichezea klabu hiyo ya Ligi Kuu kwa miezi sita, kuanzia Juni mwaka huu.


“Ochieng analijua hilo zaidi,” Kitui alisema na kuongeza: “Yeye ni mchezaji tuliye na mkataba ambaye amejiweka pabaya mwenyewe kwa kufanya udanganyifu. Nilikubali ombi la kumsajili wakati akiwa hana timu na kumpa nafasi ya kujiunga nasi.”


Mkali huyo akajiunga Leopards akitokea Rangers FC kwa mkataba usio na malipo, ambapo Ochieng akakacha mazoezi ya klabu kwa wiki mbili, kabla ya kusikia ameamua kuachana na klabu hiyo.


Ochieng mshindi wa Tuzo ya Beki Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu ya Kenya msimu uliopita, alijikuta akikosa utulivu dimbani tangu alipotimka Rangers, huku akifanya vibaya majaribio yake na klabu ya Pretoria University.


Mholanzi aliyekuwa tatbibu wa Leopards, Jan Koops naye amepigwa butwaa na kusema: “Alitoweka na kuachana nasi bila mawasiliano yoyote, jambo ambalo hatukulitarajia kufanywa na yeye.


“Simba pia ikafanya usajili wake bila kuzungumza na yeyote miongoni mwa maofisa wa klabu; badala yake, hapakuwa na taratibu zozote za kiafya kwa vipimo safi kwa mchezaji?” alihoji Koops.


Kwa mujibu wa Daily Nation, akizungumza bila kufichua jina la kiongozi, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspope ametetea uhamisho wa nyota huyo na kusema ulipata baraka za Leopards, kabla ya kumsajili na kumtambulisha rasmi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI