Wachimba migodi kufunguliwa mashtaka


Wachimba migodi wa Marikana wakigoma
Wendesha mashtaka wa serikali nchini Afrika Kusini wanasema kuwa wanajianda kuwafungulia mashtaka ya mauaji wachimba migodi wa mgodi wa Marikana.

Ripoti zinasema pia, wachimba migodi hao, wanakabiliwa na mashtaka mengine ikiwemo jaribio la mauaji ya wachimba migodi thelathini na wanne ambao waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Msemaji wa ofisi ya kiongozi wa mashtaka nchini humo, amesema ikiwa watu, ambao baadhi yao wamejihami wakiwakabili polisi na kutokee mauaji, wale watakaoshikwa na polisi watafunguliwa mashtaka ya mauaji, bila kujali wale waliofyatua risasi.

Polisi waliwapiga risasi wachimba migodi hao kufuatia ghasia na maandamano kuhusu mishahara.
Maafisa wawili wa polisi waliuawa kwenye machafuko hayo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI