*WAFANYAKAZI WA MGODI ZAIDI YA 30 WALIOKUWA WAKIANDAMANA WAMEUAWA NA POLISI NCHINI AFRIKA YA KUSINI

 Polisi wa nchini Afrika ya Kusini leo, wamewafyatulia risasi na kuwaua Waandamanaji 30, waliokuwa wafanyakazi wa Mgodi wa Platnum, wakati wakiandamana huko Kaskazini Magharibi mwa Johannesburg, wakiwa wamebeba marungu na mapanga leo mchana.

 Imeelezwa kuwa mmiliki wa Mgodi huo wa Platnum, Lonmin ndiyo hasa amekuwa chanzo cha  vurugu za wafanyakazi hao kutokana na kudai malipo, uliochochewa na mvutano baina ya vyama viwili vya wafanyakazi.

Vurugu zilizokuwa zikiendelea wakati wa mgomo huo zilisha sababisha vifo vya watu 10 kabla ya leo.
Tukio hilo la polisi kumwaga damu za wananchi ni kubwa tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
Waandamanaji hao wakiwa nje ya mgodi huo wakati wakiandamana na marungu na mapanga wakimtaka mwajiri wao kuwalipa malipo yao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA