WAKENYA 11 WAFA, 25 WAJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MANNE MKOANI PWANI

 Majeruhi wa ajali iliyohusisha magari manne, yakiwemo mabasi mawili na malori mawili katika Barabara ya Chalinze-Segera, eneo la Makole, mkoani Pwani leo, akiwa Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu. Watu 11 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa.(PICHA NA KHAMIS MUSSA)
 Wauguzi katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili, Dar es Salaam, wakimuingiza wodini mmoja wa majeruhi wa ajali iliyohusisha magari manne, yakiwemo mabasi mawili na malori mawili katika Barabara ya Chalinze-Segera, eneo la Makole, mkoani Pwani leo. Watu 11 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa.(PICHA NA KHAMIS MUSSA)

 Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo, Suzan Ngene kutoka Kenya, ambaye alivunjika mkono akiwa amefikishwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili Dar es Salaam leo, baada ya kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne, yakiwemo mabasi mawili na malori mawili katika Barabara ya Chalinze-Segera, eneo la Makole, mkoani Pwani jana. Watu 11 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa.(PICHA NA KHAMIS MUSSA)
 Muuguzi Lidarose Rutaguza akimpatia tiba Beatrice Mugwe (42), ambaye amevunjika mkono katika ajali.

WATU 11 wanaodhaniwa ni raia wa kutoka nchini Kenya wamefariki dunia papo hapo huku wengine 25 kujeruhiwa kwenye ajali iliyotokea kwenye kijiji cha Makole Kata ya Mandela Bagamoyo Pwani iliyohusisha magari manne wakiwa safarini kuelekea jijini Dar es salam kwa ajli ya uimbaji wa kwaya.

Magari hayo mawili yamegongana majira ya saa 11 alfajiri ya Agost 10 ambapo kati ya magari hayo mojawapo ni lori ambalo lilisababisha kufunga barabara na kusababisha abiria waendao katika maeneo ya Kanda ya Kaskazini kuweka kambi kwenye kijiji hicho ambapo zaidi ya masaa manane.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kwamba gari lenye namba za usajili KBQ 203 P Isuzu Bus pamoja na gari lenye namba za usajili KBL 044 M Isuzu Bus yote yakitokea nchini Kenya na kuelekea jijini Dar es Salaam yakiwa yamebeba waimbaj wa Kwaya wakiwa yamebeba waumini wa dini ya kikristo.

"Basi lenye namba za usajili KBQ 203 P lilikuwa mbele ya basi namba KBL 044 M lilikuwa likiendelea na safari bila kujua kilichotokea katika basi lingine na baada ya kupigiwa simu na wenzao iliwalazimu kuanza kugeuza gari hadi eneo lilipopinduka gari la kwanza," alisema Kamanda Mangu.

Ameongeza kwamba baada ya kufika kwenye eneo hilo abiria waliokuwa kwenye basi lililopinduka walihamisha mizigo yao na kuingia katika gari lenye namba za usajili KBL 044 M.

Ameongeza kuwa wakati abiria hao wakiendelea na utaratibu wa kuhamia gari lingine ghafla lilitokea lori lenye namba za usajili T 229 ASP Trela T785 ASX Scania likielekea jijini Dar es salam iliigonga basi lililokua limeegeshwa pembeni lenye namba za usajili KBL 044 M na kuisukuma upande wa kushoto wa barabara.

"Watu 11 wamepoteza maisha yao papo hapo kwenye ajali hiyo ambao wote ni wanawake huku wengine 25 kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili MMC ya jijini Dar es Salaam," alisisitiza Kamanda Mangu.

Kamanda huyo ameongeza kuwa baada ya kusukumwa basi hilo, lori liliendelea na safari na ndipo lilipogongana tena uso kwa uso na gari lenye namba za usajili T 272 DWZ na T 449 PVW lililokuwa likielekea mkoani Arusha na kusababisha kufunga njia kwa masaa nane.

Kamanda Mangu alisema kuwa tangu muda wa ajali jitihada zakutoa magari hayo barabarani zilikamilika majira ya saa sita mchana ndipo magari mengine yaliendelea na safari zao.

MAngu amemalizia kwa kusema kuwa ajali hiyo ni moja kati ya ajali saba zilizotokea usiku wa kuamkia Agosti 10 mkoani Pwani ambazo zimetokea katika barabara Ku za Dar es Salaam -Chalinze –Morogoro na Chalinze
–Segera.

MWISHO

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA