WANAONYANYASA WAFANYAKAZI WA NDANI KUKIONA

SERIKALI imesaini mkataba utakaowabana waaajiri wanaowanyanyasa wafanyakazi wao wa kazi za ndani.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni juzi, mjini hapa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati akihitimisha mjadala wa hotuba yake.

Alisema, baada ya kusaini mkataba huo, serikali inatarajia kuuwasilisha bungeni, ili utekelezaji wake uanze mara moja.
“Serikali imeshasaini mkataba huo na tutauleta bungeni ili ikibidi sheria ichukue mkondo wake kwa waajiri wanaowanyima chakula wafanyakazi wao na hata kuwafanya nyumba ndogo,” alisema.

Waziri Kabaka alitoa kauli hiyo, baada ya mbunge wa Chaani, Ali Juma Ali, kuhoji waaajiri wanaowanyanyasa wafanyakazi wao wanachukuliwa hatua gani, kwani wamekuwa wakipata manyanyaso makubwa.

“Wafanyakazi wa ndani wapo katika utumwa mkubwa, wengine wanatumiwa kama wanyama, hawatakiwi hata kuchanganyika na watoto wa waajiri, wanatakiwa kula chakula jikoni. Hivi hiyo TUICO ipo au imelala na kuzimia. Waziri ipatie dawa.

“Nilikutana na mfanyakazi mmoja, alipoomba msaada kwa mwajiri wake wa kumpeleka mtoto wake hospitali, alipewa mshahara wake wa siku 14 alizokuwa amefanya kazi. Alimuuguza mtoto wake, lakini bahati mbaya alifariki na aliporudi aliambiwa kuwa nafasi yake imeshajazwa. Huu ni ukatili mkubwa.

“Mbali na wafanyakazi wa majumbani, pia wafanyakazi wa hoteli wanalipwa mishahara midogo na hata wakivunja sahani watakatwa sh 10,000 kuchangia sahani moja. Pia mfanyakazi katika kampuni ya ulinzi analipwa sh 80,000 kwa mwezi na hana siku ya mapumziko. Hii ni dhulma kwa wafanyakazi,” alisema.

Akijibu suala la chama kinachoshughulikia wafanyakazi hao, Waziri Kabaka alisema kuwa si Tuico, bali ni Chama cha Chodawu na kuongeza kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho amesikia kilio hicho.


juu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.