WATU 51 WANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA MABASI MATATU MOROGORO

Jinamizi la ajali ya barabarani imeanza kugubika kwa wakazi wa Morogoro na vitongoji vyake baada ya watu wapatao 51 wamenusurika kufa baada ya mabasi matatu likiwemo lenye namba za usaji T425 BYS Utong,T692 BKV naT777 BWL kugongana na kuanguka eneo la Mkundi kwa Makunganya barabara kuu ya Morogoro -Dodoma nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro.

Kwa mujibu wa Mashuhuda wa ajali hiyo inayodaiwa kutokea saa 2:30 asubuhi na kuhusisha mabasi hayo mali ya kampuni ya Shabiby kutoka Dodoma-Dar es Salaam,Alis sport na Sumry zikitoka Morogoro-Mwanza zilitokea ghafula baada ya kuanza kuyumba na kuacha njia kisha kupinduka.
Mmoja wa majeruhi aliyekuwa kwenye basi la Shabiby Rashid Shaaban alisema muda mfupi bada ya kuanguka na kutoka ghafla waliona basi laSumry likiacha njia na kupinduka lilikuwa lilikuwa likijaribu kulipita gari jingine lilokuwa limefika maeneo hayo.

alisema kuwa kulikuwa na na watu wengi wanashangaa,hapohapo wakati wanashangaa ajali hizo na kuwaokoa watu wliokuwa kwenye mabasi haya basi la Alis sport kutoa Morogoro nalo lilipofika hapo likacha njia na kupinduka.

Hata hivyo majeruhi walisema muda mfupi baada ya ajali hiyo polisi walifika na kuanza kuwasaidia kutoka kwenye mabasi hayo kuwakimbiza hospitali ya rufaa Morogoro na kutuliza watu waliokuwa wakionekana kutaka kuweweseka na wengine kutaka kufanya uhalifu kwa mgongo wa kutoa msaada kwa abilia.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro,
ilithibitisha kupokea majeruhi 51 kati yao 28 ndio walolazwa
na kwamba hali zao zinaendelea vizuri .

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Faustine Shilogile alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa ajali hiyo imetokana na utelezi pia mwendo kasi wa mabasi hayo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI