Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe azungumza na Mabalozi wa Nje nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (katikati), akizungumza masuala mbalimbali na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini, Dar es Salaam leo, ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi Juma Mpango wa Kongo (DRC), ambaye pia ni kiongozi wa Mabalozi wa nje hapa nchini na kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Rajab Gamaha. 


Baadhi ya Mabalozi, wakiwemo Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini (EU), Filiberto Ceriani Sebregondi (kulia) na Naibu Balozi wa Ujerumani nchini, Hans Koeppel (katikati), wakimsikiliza Waziri Membe wakati  alipokuwa akizungumza nao leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya Mabalozi, wakiwemo Balozi wa Malawi, Flosie Asekanao Gomile-Subiaomba (wa tano kutoka kushoto) na Mabalozi kutoka nchi za Nigeria, Pakistani, Palestina, Rwanda, Somalia na nchi nyingine, wakimsikiliza Waziri Membe, wakati akizungumza nao leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (katikati), akizungumza masuala mbalimbali na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini leo katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi Juma Mpango wa Kongo (DRC), ambaye pia ni kiongozi wa Mabalozi wa nje hapa nchini na kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Rajab Gamaha. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.