BFT YAUNDA KAMATI YA KUSIMAMIA MASHINDANO YA TAIFA

Na Elizabeth John

SHIRIKISHO la ngumi za ridhaa Tanzania (BFT), limeunda kamati itakayosimamia mashindano ya Taifa yanayotarajia kuanza kutimua vumbi leo, katika Uwanja wa Ndani wa Taifa, ili kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha Kitaifa.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Katibu Mkuuu wa BTF, Makore Mashaga alisema kamati hiyo imeundwa kwa kuwajumuisha wataalamu wa ufundi kutoka kamati za BFT, mabondia wa zamani na wataalamu wa mipango na fedha kutoka katika taasisi na mashirika ambayo yamekuwa mstari wa mbele kusaidia kwa vitendo shughuli na matukio mbalimbali ya BFT.

Aliwataja wajumbe ambao wameteuliwa kuunda kamati hiyo kuwa ni Andrew Kweyeyana ambaye ndie Mwenyekiti wa kamati, Willy Issangura, Juma Suleiman, Remy Ngabo na Mohamed  Kasilamatwi.

Wengine ni Said Omary, Anthony Mwang’onda, Joel Magori, Charles Jilaba na Undule Mwampulo ambao wote hao waliweza kusaidia kwa namna moja au nyingine kwa bondia pekee hapa nchini, Suleiman Kidunda kuweza kufuzu mashindano ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni London, Uingereza.

“Jukumu walilopewa ni kuhakikisha mashindano yanafanyika kwa kufuata taratibu zote za zote za Chama cha Ngumi cha Dunia (AIBA) na kuhakikisha fedha za kuendesha mashindano zinapatikana na majukumu ya kamati hiyo yatamalizika baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI