DROGBA; BADO 'NIPO NIPO' SHANGHAI SHENHUA
SHANGHAI, Shenhua
“Nimeikumbuka sana Ligi Kuu ya England, kwa sababu ni
moja ya ligi kubwa na bora duniani, lakini ukweli ni kwamba, sijutii uamuzi
wangu wa kuja hapa Shanghai”
MSHAMBULIAJI Didier Drogba kwa mara ya kwanza amekanusha
tetesi zinazomuhusisha na uwezekano wa kurudi kukipiga katika moja ya klabu za
Ligi Kuu za England.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, aliihama klabu
bingwa barani Ulaya Chelsea, na kutua Shanghai Shenhua ya hapa China katika
usajili uliopita wa majira ya joto barani Ulaya.
Ukata na tatizo la kipesa lililotajwa kuikumba klabu ya
Shanghai inayoshiriki Ligi Kuu ya China, ukadaiwa kuziweka vitani klabu mbioli
za Arsenal na Liverpool katika jaribio la kupata saini ya Drogba – na sasa
kauli hii inaziweka mbali klabu hizo.
Lakini mkali huyo aliyefunga fainali na kuipa Chelsea
ubingwa wa Ulaya kabla ya kutimka ameibuka na kusisitiza kuwa anayapenda kwa
ujumla maisha ya ndani na nje ya uwanja akiwa na klabu yake mpya.
“Niseme kweli nina furaha kuwa hapa, hivyo sina hata sababu
ya kuondoka. Sitaki kabisa kuihama klabu hii.
“Nataka kuendelea kubaki hapa muda mrefu kadri nitakavyoweza,
kushinda baadhi ya mataji nikiwa na timu yangu na kuwafanya mashabiki wafurahie
uwapo wangu.
“Najua ni ngumu kutimiza ndoto hizo kwa sasa, lakini najua
kwamba kuna tumaini hilo na naamini pia kuwa nitaendelea kuwa sehemu ya kikosi
kumalizia mkataba wangu na Shanghai.
Akaongeza kuwa: “Mkataba wangu hapa ni wa miaka miwili na
nusu, labda na zaidi. Labda na zaidi na natumaini itakuwa zaidi kwa sababu nina
furaha ya kweli hapa.
Comments