TAMKO LA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA LINDI(LPC) KUHUSIANA NA MAUAJI YA DAUDI MWANGOSI
Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Lindi(LPC)kimepokea kwa masikitiko taarifa ya mauaji ya Mwandishi wa Habari wa Channel ten ambae pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Iringa, Daudi Mwangosi yanayodaiwa kufanywa na Jeshi la Polisi Mkoani Iringa tarehe 2/9/2012.
Kutokana na mauaji hayo na kutoridhishwa na nguvu kubwa kupita kiasi inayotumiwa na polisi dhidi ya raia, Waandishi wa habari Mkoa wa Lindi inaunga mkono Maandamano Makubwa yanayofanywa kimya kimya na waandishi wa Habari katika Mikoa yote Nchini na kuratibiwa Kitaifa na Jukwaa la Wahariri
Kufuatia Tukio hilo na mengi yanayowakuta Waandishi na Raia na katika kujenga dhana ya uwazi na uwajibikaji,Waandishi wa habari Mkoa wa Lindi wanamtaka Waziri wa mambo ya ndani, Mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) na Kamanda wa mkoa wa Iringa wajiuzulu nyadhifa zao kwa kuwa wameshindwa kusimamia vyema usalama wa raia na mali zao.
Pia Tunasikitishwa kwa Mfumo uliotumika wa kuunda kamati ya kuchunguza kifo hicho haupaswi kuwemo kwa wawakilishi wa Jeshi la polisi kwa kuwa wao ndio waliohusika na mauaji hayo na kwamba tume huru itakayoundwa ipewe muda maalumu ili majibu yapatikane mapema na kwa haraka na hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.
Waandishi wa habari Mkoa wa Lindi,Tunaamini kuwa Serikali na jeshi la polisi litachukua hatua stahiki kwa waliohusika na mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi, na pia Polisi watajitathmini upya katika utendaji wa shughuli zake hasa katika udhibiti wa vurugu na uzuiaji wa maandamano.
Kwa kumalizia Tunaitaka Serikali kuchukua jukumu la ,malezi ya Familia ya Marehemu Mwangosi katika kipindi chote cha mpito Ikiwa pamoja na kuwezesha watoto wake kupata elimu stahiki
Mwisho Tunalitaka Jeshi la Polisi Kutoa Ushirikiano sawa kwa Matukio ya aina zote kwa kuwa Tayari Kuna mifano iliyotokea Mkoani Lindi pale Polisi walipokuwa Wamekosa na kushikiliwa chini ya Ulinzi wa Jeshi hilo kwa Makusudi uamua kuzuia waandishi kufanya kazi zao kwa kutowapiga picha watuhumiwa ambao ni askari wa Jeshi la polisi
Hii haikubaliki na Sisi Chama cha Waandishi wa Habari Tutakuwa Tayari kuvunja Mahusiano ya Kikazi hususani katika kusaidia Mfumo unaolipatia sifa kubwa Jeshi hilo kwa Ushirikishi kupitia POLISI JAMII
MUNGU MPOKEE DAUDI MWANGOSI NA MSAMEHE MAKOSA ALIYOYAFANYA DUNIA KWA KUWA KIFO CHAKE KILIVYO NI ADHABU TOSHA
AMEEN
……………………………..
ABDULAZIZ AHMEID,
Mwenyekiti LPC.
11 September 2012

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA