IBF YAWATEUA MAKAMU WANNE WA RAIS KATIKA BARA LA AFRIKA, GHUBA ZA UARABU NA UAJEMIFriday, September 21, 2012 6:53 AM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 20/09/2012

Shirikisho la Ngumi la Kimataifa IBF limepanua wigo wake wa kusimamia na kuratibu ngumi katiuka bara lka Afrika, Mashariki ya kati, Ghuba ya Urarabu na Ghuba ya Uajemi. Katika miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa sana la vijana wengi kujiunga na ngumi na hivyo wengi kuhitaji huduma za shirikisho la IBF.

Ili kujiweka vizuri katika nafasi ya kutoa huduma nzuri inayotakikana, IBF imewateua Makamu wanne wa rais watakaomsaidia Raia wa Shirikisho hili Bwana Onesmo Ngow
 

Uteuzi huu umefuata mambo yafuatayo: Upendo wa wahusika wenyewe kwa mchezo wa ngumi, nafasi aliyonayo kwenye jamii, ukaribu wake na vijana, uwezo wake kielimu na michango yake kwa michezo.

Wafuatao wameteuliwa kuwa makamu wa Rais kuanzia mwisho wa mwezi huu:

Ayman Saad Bait-Saleem (Oman);
Makamu wa Rais, Fedha

Ayman ni mhandisi mwenye shahada ya uzamili kutoka katika chuo kikuu cha Karolina ya Kusini (University of South Carolina, Colombia South Carolina, USA.) mwa nchi ya Marekani. Amefanya kazi kama Meneja Mkuu wa bandari ya Sultan Qaboos kwa miaka mingi, Meneja wa kampuni ya APL Moller Group ya Denmark nchini Oman, Kampuni ya Marekani ya ushauri wa Kihandisi na nyingine nyingi. Kwa sasa Ayman ni mfanyabishara mwenye kampuni nyingi nchini Oman mojawapo ikiwa ni AL SWAYNI SPORT SERVICES katika jiji la Muscat, Oman

William Steven Kallaghe
Makamu wa Rais, Utawala na Masoko

William ni msomi aliyebobea katika masuala ya Uchumi na Utawala na alisoma katika chuo kikuu cha Budapest, Hungary. Ana uzoefu mkubwa kwenye masuala ya uchumi na masoko na amefanya kazi na makampuni kadhaa kama Mkurugenzi Mkuu wa benki ya kiislamu ya NBC, Meneja Miradi wa benki ya CRDB, Meneja wa Masoko wa Kanda wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kabla ya kuhamishia ujuzi wake kama Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya NBC.

Henry Mann-Spain (Ghana)
Makamu wa Rais, Operations

Henry ni mfanyabishara aliyeboboea kwenye biashara mbalimbali na analimiki makampuni makubwa ya kutengeneza bidhaa za kilimo kama nguo na vyakula vya kugandishwa (Frozen Food).

Ana Shahada ya Uzamili wa Biashara (MBA) kutoka katika Chuo Kikuu cha Harvard kilichopo katika jimbo la Massachusetts nchini Marekani. Henry amefanya kazi kwa miaka mingi na mashirika ya kimataifa yakiwamo UNHCR, ILO na UNDP.

Kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Golden Crescent Ltd yanayojishughulisha na kutengeneza bidhaa kutoka kwenye mazao ya mifugo na kilimo nchini Ghana na kuyauza nchi za Ulaya, Marekani na Asia.

Louaa Debes (Misri)
Makamu wa Rais, Ubingwa na Viwango

Louaa ni mfanya biashara anayeishi katika jiji la cairo nchini Misri na ana uzoefu nkubwa kweney masuala ya biashara za kutengeneza nguo.

Louaa Debes amesoma biashara kwenye Chuo Kikuu cha Cairo na amefanya kazi na taasisi za serikali kabla ya kuanzisha shughuli za biashara. Debes anamiliki makampouni ya ulinzi, maduka makubwa (Super markets) pamoja na kamouni ya ukodishaji wa magari.

Imetolewa na:
Onesmo A.M. Ngowi
Rais
IBF katuka bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi.
(IBF President for Africa, Middle East, Arabian and Persian Gulfs

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.