Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Taifa wa CCM,Nape Nnauye,alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari jana kuhusu Kufanyika kwa Vikao vya juu vya Chama hicho katika Ukumbi wa White House mjini Dodoma,vikijadili majina ya wagombea nafasi mbali mbali  zikiwemo,Uwenyekiti wa Wilaya na Mikoa na Ujumbe wa Halamashauri Kuu ya Taifa.
Nape  Nnauye akiwalekeza jambo waandishi wa habari wakati alipokuwa akiongea nao mjini Dodoma jana.Picha na Ramadhan othman-Dodoma
--
Na Rajab Mkasaba, 
Dodoma VIKAO vya ngazi ya juu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete vinandelea hapa mjini Dodoma vikiwa na ajenda kuu ya uchaguzi ndani ya chama hicho. 
Viongozi mbali mbali wa chama hicho wapo mjini hapa kwa lengo la kushiriki vikao hivyo akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein. Miongoni mwa shughuli kubwa za vikao hivyo ni pamoja na kuchuja majina ya wagombea walioomba kuteuliwa na chama hicho katika nafasi kadhaa zikiwemo nafasi za Uwenyekiti wa Wilaya, Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ngazi ya Wilaya na Uwenyekiti wa Mkoa.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM,inatarajiwa kuanza kikao chake kuanzia kesho na keleza kuwa kutokana na mabadiliko ndani ya chama hicho hivi sasa Wajumbe wa NEC pia,watatoka katika Wilaya.
Alieleza kuwa nafasi nyengine ni za Wenyeviti wa Mikoa, Katibu wa uchumi na fedha wa Mkoa, nafasi za U-NEC kitaifa, ambazo 10 I kutoka Bara na 10 kutoka Zanibar. Kwa upande wa Zanzibar Katibu huyo, alisema kuwa pia kuna Wajumbe wa NE wanaotoka Wilayani na Mikoani na kusisitiza kuwa tayari majina ya wagombea mbali mbali kutoka Jumuiya za Chama za UVCCM, Wazazi na UWT yameshapitiwa na hivi sasa yameshaanaliwa kwa ajili ya kusubiri vikao vya uwamuzi. Wakati huo huo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesisitiza kauli yake ya kuwa yeye yuko tayari kutoa taarifa wakati wowote zinapotakiwa taarifa hizo na waandishi. 
 Alieleza kusikitishwa na tabia ya baadhi ya vyombo vya habari vinavyotoa taarifa kutoka kwa watu wa pembeni ambao sio wasemaji wa chama hicho ambapo hatimae husababishwa kutolewa taarifa zenye utata na zenye kujikia upande mmoja. Nape aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma na kueleza kuwa ni vizuri kukaandikwa habari za uhakika na kuachana na zile habari za watu wa pembeni ambazo aghalabu huwa I habari za kutumiwa na watu. Katika maelezo yake, Nape alieleza kusikitishwa na tabia hiyo ya baadhi ya vyombo vya habari na kusisitiza kuwa yeye masaa yote 24 yuko tayari kutoa taarifa hata saa tisa za usiku. 
  “Mimi niko tayari kutoa taarifa wakati wowote na iwapo ukiandika habari ya kupewa na mtu ujue kuwa hali hiyo ndio inayosababisha makundi kwani ni taarifa za mlengo mmoja, na ukipewa nitafuate ili nikuthibitishie na hatimae upate kuandika kitu chenye uhakika wa pande zote mbili”,alisema Nape. Nape alisema kuwa kutokana na azma ya kuwarahisishia waandishi wa habari kuwa wanapata taarifa sahihi na kuzirusha kwa wakati afisi yake inampango wa kuweka karibu huduma zote za kutuma habari yakiwemo mawasiliano ya mtandao.  
Alisema kuwa yeye akiwa pamoja na maafisa wa kitengo chake wamekusudia kuchukua hatua hiyo kwa kutambua kuwa afisi yake ina dhima ya kutunza taswira ya Chama Chama Mapinduzi (CCM), hivyo kuandika habari zisizosahihi hazitokipendezesha chama chake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.