KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI CHATEMBELEA TBL

 
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kushoto) akitoa maelezo mbele ya ujumbe wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, jinsi Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), inavyotoa inavyowatahadharisha watu kutolewa wakati wakiendesha vyombo vya moto. Ujumbe huo ulialikwa kutembelea Makao Makuu ya kampuni hiyo, jijini Dar es Salaam juzi.
 
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia), akitoa historia ya kampuni hiyo kwa ujumbe wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, uliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam
 
Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano (kushoto), akiipongeza Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). kwa utaratibu waliowawekea madereva wa malori yao ikiwemo vidhithiti mwendo na muda mfupi wa kuendesha magari hayo hivyo kupunguza ajali. Kahatano aliongoza ujumbe wa askari 9 kutembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam
 Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Kuruthum Bambe akiuliza swali kwa uongozi wa TBL
 
Meneja wa Usalama mahali pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda (katikati), akitoa maelezo jinsi mitambo ya kusafisha maji taka kuwa safi, wakati ujumbe wa askari 10 wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, ulipotembelea kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi. Kulia ni kiongozi wa ujumbe huo Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano. Kutoka kushoto ni, ASP Emilian Kamuhanda na Mkaguzi wa jeshi hilo, Theresia
 
Meneja wa Usalama mahali pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda (katikati), akitoa maelezo jinsi mitambo ya kusafisha maji taka kuwa safi, wakati ujumbe wa askari 10 wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, ulipotembelea kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi. Kulia ni kiongozi wa ujumbe huo Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano. Kutoka kushoto ni, SSGT Enock Machunde, ASP Emilian Kamuhanda na Mkaguzi wa jeshi hilo, Theresia Kimaro.
 
Meneja wa Usalama mahali pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda (kushoto), akiuongoza ujumbe wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani kutembelea eneo la upishi wa bia, wakati askari hao walipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi. Kutoka kulia ni, SSGT Enock Machunde, ASP Emilian Kamuhanda na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Kuruthum Bambe na Mnadhimu Mkuu wa Kikosi hicho, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano.
 
Mtaalam wa Upishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Adolf Ndyeabura (kulia) akitoa maelezo jinsi mitambo inavyochuja bia wakati ujumbe wa askari 10 wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, ulipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi, ikiwa ni moja ya shamrashamra ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
Mtaalam wa Upishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Adolf Ndyeabura (kulia) akitoa maelezo jinsi mitambo inavyochachusha bia wakati ujumbe wa askari 10 wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, ulipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi, ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.