KUAPISHWA KWA MNADHIMU MKUU WA JESHI (JWTZ) NA MKUU WA JKT


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atamuapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Samuel Albert Ndomba na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Raphael Mugoya Muhuga, kesho Jumatano tarehe 26 Septemba, 2012, katika viwanja vya Ikulu, katika muda utakaotangazwa baadaye.

"Kwa kuzingatia umuhimu wa shughuli hii, Nawaomba wahariri mtutumie jina la mwandishi na mpigapicha ambao watafika Ikulu kwa ajili ya shughuli hii. Kwa umuhimu wa maandalizi ya shughuli hii, tunaomba majina ya wawakilishi wa vyombo vyenu yawasilishwe kwetu leo Jumanne 25, Septemba, 2012", imesema taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasilino ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.

 "Tunapenda kusisitiza kuwa waandishi watakaoruhusiwa kuhudhuria shughuli hii ni wale tu ambao tutapokea majina yao kutoka kwa wahariri wa vyombo husika. Aidha, tunasisitiza mavazi yawe nadhifu na heshima, kwa kuwa hii ni shughuli ya Kitaifa. Tunaomba ushirikiano wenu na karibuni", Taarifa hiyo imeongeza.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.