KUMBUKUMBU YA MIAKA 5 YA MZEE S T NATHAN (BABA WA FATHER KIDEVU)

Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika mitano sasa imetimia tangu Mzee Shauri Timoth Nathan
 (18/08/1925-18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama ulivyotutangulia kuja duniani Tarehe 18/09/2007 saa kumi na mbili jioni.

Nimajonzi sana kwetu hasa ukizingatia kuwa uliondoka katika tarehe ambayo kitinda mimba wako Mroki Mroki alizaliwa na ni siku kumi tu baada ya kufunga ndoa Mroki “Father Kidevu”.

Unakumbukwa na wengi sana maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee ni Mke wako Mary O Nathan na watoto wako James Nathan, Mrs Stella Kaluse, Lloyd Atenaka, Dossa Mroki,Freddrick (Kajiru) Mroki, Onesmo Nathan, Thomas Nathan, Daniel Nathan, Kyaze Nathan, Namche Mroki, Kille Nathan na Mroki Mroki na Wakwe zako wote.

Pia unakumbukwa sana na Wajukuu zako Kidai Kaluse, Shauri Kaluse, Mfaume Kilangi, Shauri James, Mwanaamani James, Hellena James, Nuru James, Maria Kaluse, Ludao Kaluse, Kilave Atenaka, Maria Atenaka, Victoria Dossa, Doureen Atenaka, Erick Mushi, Beatrice Mroki, Timothy Tomas, Timothy Kajiru, Imanuel Kajiru, Eliewaha KajiriTimothy Kille, Maria Thomas Irine Atenaka, Anjela Chistian, Glory Mroki, Nathan Kyaze, Nathan Dossa, Dinner Onesmo,Digna Onesmo, Debora Daniel na  Leonard Kyase pamoja na Vitukuu wako pia kutoka kwa Mwanaamani na Shauri.

Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kipera , Kitongoji cha Kinyenze,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia wanakukumbuka sana.
Tunakumbuka maneno yako ya Mwisho uliotuachia watoto wako kuwa “TUPENDANE, TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE,” baba hakika hili linatendeka na tupo na umoja uliotujengea na tunajivunia hilo.

Tunazidi kukuombea Baraka na pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufata kama tulivyo kufuata hapa duniani.

Jina la Bwana Lihimidiwe Amina

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.