Lipumba achambua uchumi wa dunia, aonyesha njia kuelekea mafanikio.



 Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF, Prof.Ibrahim Lipumba akiwasili kwenye Mkutano wa Chama hicho uliofanyika Jangwani jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wananchi na wanachama wa chama hicho waliojitokeza kwenye mkutano huo.

 Wafuasi wa Chama hicho wakifurahia jambo.
 Kikundi cha Mchiriku nacho hakikua mbali kutumbuiza.
 Kadi za vyama mbalimbali zilirejeshwa na kukabidhiwa kadi mpya.
 Afande Sele nae alitumbuiza kwenye mkutano huo.

 Msanii Kala Pina, akitoa burudani kwa wanachama wenzake wa chama hicho, kwenye uchaguzi wa 2010, Kalapina aligombea udiwani kupitia chama hicho kwenye kata ya Kinondoni.
 
KATIKA kile kinachoonekana ni kujipanga kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Chama cha wananchi CUF leo kimezindua mkakati mpya wa kujiimarisha nchi nzima. 
 
Akiwahutubia maelfu ya wanachama waliohudhuria kwenye mkutano mkubwa Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba pamoja na mabo mengine ya kiuchumi wa dunia na wa hapa nchini lakini hakuacha kugusia mkakati wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015.
 
Alisema chama chake kimejipanga kimkakati kuelekea uchaguzi huo na anaamini watanzania watakiunga mkono kwani ni ndio chama pekee chenye sera mbadala za kuleta mabadiliko. Aidha Prof. Lipumba alisema uchumi wa dunia kwasasa uko katika halimbaya sana lakini hali mbaya hiyo inatoa fursa kwa nchi masikini kujiimarisha kupitia kilimo kutokana na bei ya mazao ya kilimo kuongezeka duniani kote.
 
Aidha Lipumba alifafanua kuwa kuongezeka kwa mahitaji ya mazao ya kilimo kunatokana pia na kuimarika kwa uchumi kwenye nchi ambazo zina watu wengi akitoa mfano wa China na India ambazo zinawatu zaidi ya bilioni moja .
 
Awali akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo Naibu Mkurugenzi wa habari na uenezi wa Chama hicho Abdull Kambaya, alisema tabia ya chadema ya kuisema CUF kama ni CCM B, ni yakuficha ukweli kwamba wao ndio CCM B kwa kuendesha chama chao chini ya misaada ya makada wa CCM akiwamo kada maarufu wa chama hicho Mustafa Sabodo. Hata hivyo akahoji kuwa kitendo cha chama hicho kwenda kuombaomba CCM kupata wagombea ni kitendo cha kutojiamini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.