MABINGWA WA KAGAME YANGA WALIPOTEMBELEA KAMPUNI YA BIA (TBL)

 Mfanyakazi katika Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Adolf Ndyeabura (aliyevalia fulana ya Yanga kulia) akiwaonyesha kocha wa timu ya Yanga, Thom Sainfiet, na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo jinsi bia zinavyopikwa jana Alhamisi, wakati timu hiyo yenye maskani yake katika mitaa ya Twiga/Jangwani jijini, ilipofanya ziara yake katika kiwanda hicho kilichopo Ilala, jijini Dar es Salaam.
 

 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kushoto) akiwa na beki mpya wa timu ya Yanga, Mbuyu Twite (katikati) na Msemaji wa timu hiyo, Louis Sendeu jana Alhamisi wakati timu hiyo yenye maskani yake makutano ya Mitaa ya Twiga/Jangwani jijini Dar es Salaam ilipofanya ziara katika kiwanda hicho. Anayeonekana nyuma yao ni kocha wa timu hiyo, Thom Sainfiet.
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kushoto kabisa) akiwa na baadhi ya viongozi wa vitengo mbalimbali vya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) pamoja na wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu ya Yanga juzi Alhamisi wakati mabigwa hao wa Kombe la Kagame walipotembelea kiwanda cha TBL kilichopi Ilala jijini Dar es Salaam.
 


Wachezaji wa timu ya Yanga pamoja na Benchi la Ufundi la timu hiyo, pamoja na baadhi ya viongozi wa timu wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wanawake wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) jana Alhamisi wakati timu hiyo ilipofanya ziara kiwandani hapo, Ilala jijini Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM, Tanzania

MABINGWA wa Kombe la Kagame Yanga, jana wamefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia nchini (TBL), kilichopo Ilala jijini Dae es Salaam, ambacho kinaidhanmini klabu hiyo kupitia bia ya Kilmanjaro,.
Akiongea katika ziara hiyo, Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema timu yake iliamua kufanya ziara yao katika kiwanda hicho, ili kuweza kujionea mambo mbalimbali ambayo yanafanywa na kampuni hiyo inayozalisha vinwaji mbali mbali, ikiwamo Kilimanjaro.

Alisema kuwa, Kilimanjaro Premium Lager imekuwa ikiwapa ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa mambo mbalimbali ya kimichezo, ikiwa ni pamoja na kuwapatia magari ya usafiri jezi pamoja na vifaa, na kwamba wamefurahishwa na aina ya mapokezi waliyoyapata kiwandani hapo na kuwaomba waendelee na moyo huo huo wa kuthamini timu yao.

"Tunawaomba muendele na moyo huo huo kwani sisi kama Yanga, tunaamini kuwa huwezi kutenganisha mafanikio ya klabu yetu kwa sasa na udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager, na kwamba kwa pamoja, tutaweza kulifikisha soka la Tanzania katika kilele cha ubora," alisema Sendeu.

Awali, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kuwa wamefurahishwa sana na kitendo cha Yanga kuamua kuacha shughuli zao na kutembelea kiwanda chao, kujionea kazi za uzalishaji zinavyofanywa kiwandani hapo.

Alisema kuwa Kilimanjaro Premium Lager inathamini mchango wa timu ya Yanga katika maendeleo ya soka la Tanzania na ndio maana imekuwa ikiidhamini timu hiyo, huku akibainisha kuwa wataendela kuidhamini kwa muda mrefu kadri iwezekanavyo.

Thamani ya udhamini wa Kilimanjaro kwa Yanga unafikia jumla ya dola za Kimarekani 1.5milioni (Shillingi Bilioni mbili za Kitanzania) kwa mwaka. Pesa hizi hutolewa kwa ajili ya shughuli mbali mbali kama kusajili wachezaji wapya wa kimataifa, mabasi, vifaa vya michezo na kukiwezesha Mkutano Mkuu wa Mwaka.

"Tunafanya hivi tukiwa na nia ya kupeleka soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio… Ni dhahiri kuwa Yanga imekuwa ikifanyia mambo makubwa kwani imekuwa ikiwapatia vijana mbalimbali ajira kupitia timu yao. 

"Ushirikiano wetu na Yanga unatokana na ukweli kwamba, ni kati ya timu zenye wapenzi wengi zaidi hapa nchini," alisema Kavishe

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*