MAHAKAMA KUU NCHINI CHINA YAMHUKUMU KIFUNGO CHA MIAKA 15 JELA ALIYEKUWA MKUU WA POLISI

Mkuu wa zamani wa Polisi nchini China Wang Lijun, akiwa mahakamani wakati wa kesi yake
REUTERS/CCTV.
 
Na Emmanuel Richard Makundi
MAHAKAMA kuu nchini China imemuhukumu kifungo cha miaka kumi na mitano jela aliyekuwa mkuu wa Polisi, Wang Lijun baada ya kumkuta na hatia ya makosa manne aliyoshtakiwa nayo.

Kwenye mji wa Chengdu kusini mwa nchi hiyo imemkuta na makosa ya kushiriki vitendo vya rushwa ikiwemo kuficha uchunguzi kuhusu kifo cha mfanyabiashara raia wa Uingereza aliyewekewa sumu na mke wa mwanasiasa maarufu nchini humo Bo Xilai.

Kwa mujibu wa shirika la habari la nchi hiyo la Xinhua lilisema kuwa kulingana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo umeonesha dhahiri, Lijun akiwa kama mkuu wa Polisi wakati huo kushiriki kuficha ukweli kuhusu kesi ya mauaji iliyokuwa inamkabili Gu Kailai mke wa mwanasiasa Xilai.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa Lijun akiwa rafiki wa karibu wa Xilai alishiriki moja kwa moja kufuta ushahidi wa mauaji ya mafanyabiashara Neil Heywood ambaye aliuawa kwa kuwekewa sumu baada ya kutokea kutoelewana baina yake na familia ya Xilai.

Mke wa kiongozi huyo alihukumiwa kifungo cha maisha jela mwezi wa nane mwaka huu baada ya kukiri kuhusika na kifo cha mfanyabiashara Heywood.

Chama tawala nchini humo cha Kikomunist kinatarajiwa kuamua hatma ya mwanasiasa Bo Xilai iwapo akabiliwe na mashtaka au la, kwenye uamuzi ambao utaamua hatma ya kisiasa ya mwanasiasa huyo mkongwe mwenye mvuto wa kipekee ndani ya chama hicho.

Wang mwenyewe amesema hatokata rufaa kutokana na hukumu hiyo.
You might also like:

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU