MAKUNDI YA KIISLAM YADAIWA KUPANGA MAANDAMANO YA KUMNG’OA SHEIKH MKUU.

Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaban Bin Simba
Na Datus Boniface.
Makundi ya waumini wa dini ya Kiislam wamepanga kufanya maandamano makubwa kwa lengo la kumng’oa Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaban Bin Simba

Hatua hiyo inadaiwa kutokana na kutokuwa na imani na Mufti ambaye amekaa madarakani kwa  muda mrefu huku Katiba ikimpa mamlaka ya kushika kiti hicho hadi pale atakapofariki.

Akizungumzia na waandishi wa habari katika ofisi za Bakwata, Ofisa Habari Shaban Simba, amekiri kupata taarifa hizo na kusema wamejipanga kukabiliana na lolote kutoka kwa kundi hilo la Waislam.

“Tumejipanga kukabiliana na hao wanataka kumn’goa kwa nguvu Mufti, lakini tunaomba jeshi la Polisi kuwadhbiti watu hawa” amesema.

Amesema wenye uwezo wa kumwondoa Mufti madarakani ni makubaliano maalum  ya mabaraza mbalimbali ya kiislam yaliyoketi kujadili suala la kutokuwa na imani na Mufti na si vinginevyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI