Mamia Wamlilia Mwandishi wa Habari, Agnes Yamo: Aagwa Leo

Mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima, Agness Christopher Yamo umeagwa leo mchana Buguruni, Dar es Salaam, tayari kwa safari ya mazishi kesho mjini Morogoro. Yamo aliyewahi pia kufanya New Habari 2006 Limited, alifariki dunia jana katika hospitali ya Jeshi, Lugalo, Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Katika uagwaji wa mwili wa marehemu, aliyekuwa mcheshi na rafiki wa wengi, mamia walijitokeza na wengi walishindwa kujizuia kiasi cha kulia hadi kupoteza fahamu. Hakika ilikuwa huzuni, simanzi na majonzi eneo la tukio. Agness ameliza watu. Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu, Amin. PICHA KWA HISANI YA BIN ZUBERY BLOG














Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda



Mkurugenzi wa Free Media, Lillian Mbowe

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA