MAREKANI YAIMWAGIA TANZANIA BILIONI 3,200 ZA UKIMWI

 Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, alipokuwa akizindua mkakati wa kuwarejesha kwenye huduma watu waishio na na Virusi vya Ukimwi (VVU) waliosajiliwa kutumia huduma mbalimbali za VVU na kisha kuacha kutumia huduma hizo, Dar es Salaam

Watu wa Marekani kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa nchi hiyo (PEPFAR) wamechangia dola bilioni 2 kwa ajili ya kupambana na VVU na UKIMWI nchini.

Hayo yameelezwa leo asubuhi na Balozi wa Marekani nchini,Bw. Alfonso Lenhardt, alipokuwa akizindua mkakati wa kuwarejesha kwenye huduma watu waishio na VVU waliosajiliwa kutumia huduma mbalimbali za VVU na kisha kuacha kutumia huduma hizo.

Akizindua mkakati huo ujulikanao kama ‘TUNAJALI Afya yako, Rejea kwenye Tiba,” leo asubuhi kwenye Kituo cha Afya cha Ipogolo kilichopo Manispaa ya Iringa, Balozi Lenhardt amesema kuwa asilimia 25 ya watu walioandikishwa kutumia huduma hizo hawajuliakani walipo na mkakati huu unawalenga kuwatafuta walipo warejee kwenye tiba kwa ajili ya afya na ustawi wao.

Akizindua mkakati huo, Balozi Lenhardt amesema kuwa afya ya Watanzania ni moja ya vipaumbele vya juu sana vya Marekani na kwa mantiki hiyo watu wa Marekani walishirikiana na Tanzania kuanzisha program ya kitaifa ya huduma na tiba za VVU/UKIMWI mwaka 2003 kukabiliana na janga hilo.

Balozi huyo amesema kuwa tangu wakati huo, Marekani imeongeza msaada wake katika eneo hilo ambapo mpaka sasa watu wa Marekani wametoa Dola bilioni mbili. Hatua hii umesaidia kuongeza huduma kwenye zaidi ya 700 yanayotoa huduma na tiba za VVU/UKIMWI.

Alisema hali kadhalika hatua hiyo imewezesha watanzania zaidi ya 300,000 kutumia dawa zinazopunguza makali ya VVU na hivi sasa zaidi ya Watanzania 525,000 hupokea matunzo na huduma mbalimbali.

Mkurugenzi wa Programu ya TUNAJALI inayofadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia PERFAR, Dk Gottlieb Mpangile, amesema mkakati unalenga kuwarejesha kwenye tiba zaidi ya watu 23,000 wenye maambukizi ya Ukimwi katika mikoa ya Iringa na Njombe.

Alisema watu hao ni kati ya watu 64,539 ambao mpaka Juni mwaka huu walikuwa wameandikishwa kwa ajili ya matumizi ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARVs).

“Hatujui waliko watu 23,000 wanaoishi na VVU. Tunaambiwa kuwa wengine wamefariki, wengine wamehama vituo na wengine hawaonekani kwenye tiba za ARV kwa sababu mbalimbali, lakini lengo letu ni kuwatafuta hapa na kuwarejesha kwenye tiba ili waweze kuwa na afya,” anasema Dk. Mpangile.

Awali Mratibu wa Ukimwi wa Mkoa wa Iringa, Dk Paul Luvanda alisema katika kipindi cha Julai 2011 hadi Juni 2012 jumla ya vituo 118 kati ya vituo 439 vilitoa huduma za ushauri nasaha na upimaji wa VVU.

Alisema watu 51,547 walipima afya zao katika vituo hivyo na kati yao 5,457 sawa na asilimia 10.6 walikuwa na maambukizi ya VVU.
 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.