MCHEZO WA MASUMBWI, TAA INAYOZIZIMA – SEHEMU YA NNE
Na Onesmo Ngowi
Masumbiwi
au kwa majina mwengine ndondi au ngumi na kwa majina ya mitaani ndogwa, mawe
n.k. ni mchezo unapoendwa sana na watu wengi. Aidha mchezo huu ni kati ya
michezo inayoogopwa sana duniani. Mchezo wa ngumi uko hatarini kupoteza maana
yake ya asili yaani kucheza kama burudani, kuwakilisha nchi na kujenga ushupavu
wa mchezaji. Mamilioni ya watu wanaojazana kuutazama wasingependa kabisa
kujiingiza kuucheza mchezo wa ngumi. Sasa
endelea………………………………….!
MATUMIZI YA SHERIA MPYA ZA NGUMI
Ni
katika mwaka 1866 wakati ambapo mtawala wa Queensbury (Marguees of Queensbury)
huko Uingereza alisaidia kutunga sheria mpya zilizotumika kuuendesha mchezo wa
ngumi sheria ambazo kwa heshima zilipewa jina lake. Sheria hizi ziliweka bayana
mambo yafuatayo:
Uzito wa
kila bondia ulianzia Fly ambao ni chini ya kilo 50, bantam kilo 54,
featherweight kilo 57, lightweight kilo 60, welterweight kilo 67, middleweight
kilo 75, light heavy kilo 80 na hevyweight uzito ambao haukuwa na
kikomo.
Sheria
za ulingoni: zilipunguza
muda uliotumika kwenye raundi za mpambano wa ngumi kuwa dakika 3, na pia
ziliweka kikomo kwa mabondia kuangushana chini kama wacheza mieleka. Zilifanya
pia matumizi ya gloves kuwa ya lazima. Uzito wa glovu nao ulianzia oz 8, 9, 10,
12 na 15.
Pamoja na
ukweli kwamba sheria hizi mpya za hazikuweza kuzuia kwa mara moja kupigana kwa
kutumia mikono mitupu (bare-knuckle). Ushindi wa bondia maarufu wa Kingereza
James J. Corbet dhidi ya bingwa maarufu aliyejulikana kwa kucheza kwa mikono
mitupu John L. Sullivan mwaka 1892 ndipo matumizi ya gloves yalipoanza kutumika
rasmi katika mapambano yote ya ngumi.
Katikati
ya karne ya 20 kuelekea kwenye karne ya 21 sheria mpya za ngumi zilitungwa baada
ya kuanzishwa kwa mashirikisho mbalimbali ya ngumi ambayo kila moja lilikuja na
sheria zake. Kwa uchache sheria hizi zilipunguza raundi za ngumi mpaka kufikia
15 kwa ubingwa wa ngumi na kuweka sheria kali za sehemu ambazo bondia anaweza
kumpiga mwingine.
Aidha
sheria hizi ziliweka kikomo katika uzito mbalimbali ambapo kulianzishwa uzito
kama light fly, fly, super fly, light welter, junior middle, super middle n.k.
Vile vile sheria hizi mpya zilizuia matumizi ya madawa mbalimbali ya kuongeza
nguvu kwa mabondia.
Katika
mashindano makubwa ya kimataifa hususan Olimpiki wakati wa ngumi za ridhaa
sheria za matumizi ya madawa ya kuongeza ngumi ziliwekewa kipaumbele. (Wakati
huu madawa mengi ya kuongeza nguvu yamepigwa marufuku karibu katika michezo
yote).
Aidha
mabondia mbalimbali ambao waligombea mikanda ya ubingwa walitakiwa walingame
uzito na aliyezidi ilibidi apewe muda maalum wa kuupungunza hadi afikie uzito wa
mwenzie.
Ni
mwishoni mwa karne ya 20 ndipo mashindano makubwa ya utitiri wa mashirikisho ya
ngumi hususan ngumi za kulipwa yalipoanzishwa kwa fujo za aina
yake.
Mwanzoni
kulikuwepo na shirikisho moja tu nalo lilikuwa Chama cha Ngumi duniani (WBA).
Baada ya muda wa miongo kadhaa Baraza la Ngumi Duniani (WBC) nalo lilianzishwa.
Mwanzoni mwa miaka ya 80 Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) nalo
lilianzishwa.
Sababu
kubwa ambazo zinatajwa na watu mbalimbali za kuwepo kwa utitiri wa mashirikisho
haya ni ubinafsi. Lakini ukiangalia kwa makini kuanzishwa kwa mashirikisho haya
kumeweza kwa kiasi kikubwa kuwapa nafasi mabondia wengi kujulikana
kimataifa.
Hebu
fikiria kuwa katika nafasi ya ubingwa wa shirikiso moja kuna nafasi 17 tu za
ubingwa. Kwa maana nyingine mabondia 17 tu ndio wanatakiwa wajulikane kuwa ni
mabingwa wa dunia kwa wakati mmoja.
Idadi
kamili ya mabondia walioko dunia nzima haijulikani lakini inaweza kufikia malaki
kama sio mamilioni kadhaa. Itakuwa vigumu sana kwa mabondia wote kuweza kufikia
ubingwa wa dunia katika maisha yao kama kungekuwepo na shirikisho moja
tu.
Japokuwa
kuna hisia kuwa mashirikisho mengine yamezidiwa umaarufu na mengine lakini
kunasaidia kuwapa nafasi nzuri mabondia wengi kujulikana duniani. Kwa sasa
inakadiriwa kuweko kwa mashirikisho kama 15 na ukizidisha kwa 17 utaona tayari
mabondia wengi zaidi wanaweza kuwa mabingwa wa dunia kwa wakati mmoja. Japokuwa
bingwa mmoja wa dunia anaweza kujulikana kwa zaidi ya shirikisho
moja.
SHERIA ZA BAADHI YA MASHIRIKISHO YA NGUMI
Mashirikisho
mengi ya ngumi yanatumia sheria zinazofanana. Yote yanatumia sheria za “Marguees
of Qunensbury” yaani mabondia wapigane wakiwa wamevaa glovu mikononi zenye
uzito unaofanana. Wawe na uzito sawa na ngumi zipigwe kuanzia juu ya
mkanda.
Ikumbukwe
kuwa mengi ya mashirikisho haya yalianzishwa miaka ya karibuni. Kabla ya
shirikisho hata moja la ngumi kuanzishwa ngumi zilikuwa zinatawaliwa
(zinaendeshwa) na kamisheni za mitaa, manispaa na nchi mbalimbali. Hata wakati
mabondia wa zamani wanatwa ubingwa wa dunia kwao hakukuwa na njia mbadala ya
kuwakutanisha na mabondia wengi waliokuwa kwenye viwango vimoja na wanotoka
katika nchi mbalimbali.
Ikumbukwe
pia kwamba neno ubingwa wa ngumi linamaanisha ushindi wa tuzo katika kiwango
chako. Kama unawashinda mabondia karibu wote walio kwenye kiwango chako unakuwa
bingwa wa kiwango hicho. Viwango huwekwa na mashirkisho yanayosimamia
ngumi.
Kwa mfano
mabondia wanaowekwa kwenye viwango fulani vya ngumi wanatakiwa wawe wamecheza
mapambano kadhaa yenye hadhi ya kitaifa na kimataifa.
Shirikisho
la Ngumu la Kimataifa (IBF) linataka walio kwenye viwangio vyake wawe
wameshindana na mabondia wenye hadhi ya kimataifa. Viwango vya IBF vinaanzia
1-15 kila uzito. Bondia
anayeingizwa kwenye viwango vya IBF ni lazima awe amecheza mapambano zaidi ya 15
yenye hadhi ya kimataifa ya kushinda asilimia 75 ya mapambano
yote.
Yapo
mashirikisho mengine yenye utaratibu tofauti na wa IBF na ambayo masharti ya
kuingizwa kwenye viwango vyake sio magumu sana. Pengine ndio maana mashirikisho
ya IBF, WBA, WBC na WBO yanaheshimika zaidia duniani kwa kuwa masharti ya
kuwekwa kwenye viwango vyake na kucheza ubingwa wake ni magumu
zaidi.
Kwa ajili
ya sheria kuwa ngumu mashirikisho haya yana makubaliano ya kuwaruhusu mabondia
kucheza ubingwa unaotambuliwa na mashirikisho yote manne kwa pamoja (unification
titles). Yaani bondia anaweza kugombania ubingwa mmoja unaotambuliwa na IBF,
WBA, WBU na WBO na kuvaa mikanda minne. Mabingwa hawa wanajulikana kama
undisputed champions (mabingwa wasiopingika)
Sina
maana kwamba ubingwa wa mashirikisho mengine hauna maana bali yamezidiana kwa
umaarufu na heshina tu. Bingwa wa dunia ni bingwa kwa wapenzi wake na wapinzani
wake.
Wako
mabingwa wa mashirikisho mengine kama IBA, IBC, WBF, WPBF ambao wamekuja baadaye
kuwa mabingwa wa sasa wa WBC, WBA, IBF na WBO. Mfano mmoja ni bingwa wa sasa wa
WBC Vitali Klitschko toka Ukraine ambaye kwa muda mrefu alikuwa bingwa wa dunia
wa WBO. Iaendelea………………………….!
Mwandishi
wa makala haya ni; Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC),
Shirkisho la Ngumi za Kulipwa Afrika Mashariki na Kati (ECAPBF), Shirikisho la
Ngumi la Kimataifa bara la Afrika, Masharilki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi
(IBF/AFRICA) na Mkurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC)
E-mail: ibfafrica@yahoo.com
Comments