Mkono: CCM patachimbika


MBUNGE wa Musoma Vijijini, ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nimrod Mkono (pichani), amesema kama jina lake halitarejeshwa katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Taifa, patachimbika.

Mkono alitoa kauli hiyo jana baada ya kusoma kwenye vyombo vya habari kuwa jina lake limeenguliwa katika kinyang’anyiro hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkono alisema ni haki ya Chama chake cha Mapinduzi (CCM), kuondoa jina lolote kuwania uongozi, lakini haamini kama wamemuengua kwani hajaambiwa wala kupata nafasi ya kujitetea.
Alisema ana imani na CCM, lakini alionya kuwa kama ameenguliwa atapambana huko huko mpaka kieleweke.

“Ntaminyana huko huko mpaka kieleweke. Siamini chama changu tukufu kama kinaweza kufanya hivyo, siamini kwa kuwa nimejenga shule nzuri. 

Jumuiya ya wazazi kazi yake ni shule tu. Ni wahuni wachache wamekuja kusema Mkono kafukuzwa,” alisema Mkono.

Alisisitiza kuwa hawezi kuenguliwa kwani nafasi anayoomba inahusika na usimamizi wa shule na yeye ana uzoefu na masuala ya shule kwani anamiliki shule nyingi binafsi katika jimbo lake.

Mbunge huyo aliendelea kufafanua kuwa katika chama chake kuna utaratibu ambao kama mgombea hakuridhishwa anaweza kukata rufaa ya kupinga matokeo hayo na akilazimika atakata rufaa.

Alikiri kuwa mara nyingi chaguzi zinazofanyika iwe ndani ya chama au nje, huwa zina kasoro na kwamba hakuna uchaguzi usio na upungufu duniani hivyo anasubiri hatma yake kwani bado hajapewa taarifa rasmi ya kuenguliwa.

Hii ni mara ya pili kwa Mkono kuenguliwa katika kinyang’anyiro hicho. Mara ya kwanza jina lake lilienguliwa katika kikao cha Halmashauri Kuu (NEC), chini ya Rais Jakaya Kikwete kwa sababu ambazo hadi leo hazijaelezwa.

Juzi gazeti moja la kila siku liliripoti kuwa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi (CCM), imepitisha majina matatu ya wagombea ambao watawania nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya hiyo taifa, huku Mkono akiwa miongoni mwa waliotupwa nje.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa uteuzi huo ulifanyika wakati baadhi ya wagombea walioshindwa wakiibua tuhuma nzito dhidi ya wale walioteuliwa kuwa wamepita katika mazingira ya rushwa, ambao ni Abdallah Bulembo, Martha Mlata na John Barongo.

Mbali ya Mkono, wengine waliotupwa ni John Machemba, Alphonce Mwambeleko, Marley Mgasa, Jasson Rweikiza, Salim Chicago, Saidi Bwanamdogo, Muzamill Kalokola, Maseke Makono na Mosha Conrad.

Kwa maelezo ya taarifa hiyo majina hayo yaliyopitishwa yatajadiliwa katika kikao cha Kamati ya Maadili na baadaye Kamati Kuu kabla ya kupigiwa kura na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa katika matokeo hayo Mkono alishika nafasi ya mwisho kati ya wagombea wote 13 walioomba nafasi hiyo. Chanzo;Tanzania Daima

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.