MKUTANO WA 58 WA WABUNGE WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA (CPA) WAFUNGULIWA RASMI MJINI COLOMBO,SRI LANKA

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili katika ukumbi wa MNelum Pokuna Mahinda Rajapaksa kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) uliofunguliwa leo na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa. Aliye pembeni yake ni Mjumbe wa CPA Tawi la Tanzania na Mbunge wa Kigoma Mhe. Zitto Kabwe.
Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa akihutubia Maspika, Wabunge na maafisa zaidi ya 850 kutoka Mabunge ya nchi wanachama jumuiya ya madoloa wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano huo.
Spika wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akifuatilia kwa umakini ratiba ya ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) kabla ya ufunguzi rasmi leo Mjini Colombo Sri, Lanka, aliye kushoto kwake ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pande Ameir Kificho na Mhe. Zitto Kabwe na aliye kulia ni Mhe. Mussa Azzan Zungu. Mkutano huo umefunguliwa rasmi leo na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Mahinda Rajapaksa.
Spika wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akiteta jambo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pande Ameir Kificho pamoja na Mhe. Zitto Kabwe wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) leo Mjini Colombo, Sri Lanka. Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa. Wa Kwanza kulia ni Afisa dawati wa CPA tawi la Tanzania Ndg. Said Yakubu.
Mhe. Zitto Kabwe akiteta jambo na Mbunge toka Uganda (hakufahamika jina mara moja) pamoja na Spika wa Bunge la Malawi Mhe. Henry Chimundu Banda (katikati) mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa CPA unaofanyika nchini Sri Lanka. Kulia ni Mhe. Hamad Rashid Mjumbe wa CPA tawi la Tanzania.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akishangaa jambo wakati wakiwa katika mazungumzo na Spika wa Kenya Mhe. Kenneth Marende mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa CPA unaofanyika nchini Sri Lanka.
Wajumbe wote wa Mkutano wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi leo.Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.