MKUU WA MKOA WA LINDI AONYA WANASIASA KUINGILIA USHIRIKA.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila akifungua Mkutano mkuu wa 18 wa chama kikuu cha Ushirika mkoa wa Lindi unaofanyika Wilayani Liwale hii leo.
Wanachama wa chama kikuu cha Ushirika wakisiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi katika Mkutano mkuu wa 18.
Maafisa Ushirika wa wilaya za mkoa wa Lindi nao wakiwa katika mkutano huo.

Mkuu wa mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuacha kuingilia utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwa pamoja kukataa bei nzuri zinazoletwa na wanunuzi kuhusiana na mauzo ya mazao ikiwa pamoja na kushawishi wanajamii kukataa kuuza mazao yao kwa vyama vya msingi huku wengine wakiwa na maslahi yao kwa kuwanyonya wakulima ili wasipate bei ya juu.

Aidha akisoma taarifa katika mkutano huo.Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Lindi.Kilian Kapamba aliwataka wanachama wa chama hicho kubaini mapungufu yaliyojitokeza katika ununuzi wa zao la Ufuta msimu uliopita ikiwa pamoja na bei kuwa kubwa Wakulima waliibiwa kutokana na vipimio visivyothibitisha na kuwapunja wakulima,Vyama vya msingi na ushirika kukosa mapato,Kutopatikana na takwimu sahihi ya uzalishaji na kufuatia hali hizo aliiomba serikali itilie mkazo mfumo wa stakabadhi ghalani kufuatia mafanikio makubwa yanayopatikana tofauti na soko huria.
PICHA NA HABARI AHMED ABDULLAZIZ LINDI.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.