MSHINDI WA TIGO BEATS AKABIDHIWA KITITA CHAKE.

Mkazi wa Kijiji cha Kigugu, Kata ya Sungaji, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Hamis Athuman Pita (19), ( kushoto ) akipokea hundi ya mfano yenye thamani ya Tsh.10Millioni, kwa Msimamizi wa Kampuni ya Tigo Kituo cha Morogoro Neema Mashingia, anayehudumia pia na Mikoa ya Dodoma, Iringa,
Mbeya na Ruvuma baada ya kijana huyo kushinda shindano la promosheni ya Tigo Beats, iliyoendeshwa na Kampuni hiyo kuanzia Mei 21 hadi Julai 19 mwaka huu, ( kati kati) ni Mfanyakazi wa Tigo Morogoro,Vissa Majitaka.
 Hamisi athumani akiwa na mfano wa chekiyake mara baada ya kukabidhiwa.
Msimamizi wa Tigo Morogoro Neema Mashingia akizungumza mara baada ya kumkabidhi Mshindi huyo hundiyake.

TIGO metoa  zawadi kwa mshindi wa pili na wa mwisho  wa droo ya ‘Tigo Beats.’ Hamisi Athumani kutoka Turiani Morogoro ndiye mshindi wa shilingi 10,000,000/= aliyepatikana wiki iliyopita katika  bahati nasibu  iliyofanyika kwa mfumo wa kompyuta chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Bahati nasibu.  
 
“Tunajitahidi kutoa huduma bora ambazo tunataka ziboreshe maisha ya wateja wetu,” alisema Alice Maro, Afisa uhusiano wa Tigo. “Kwa sababu  ya maendeleo  ya kiteknolojia, tunataka kuwa  pamoja katika maisha ya wateja wetu kila siku na kuwa sehemu ya mafanikio yao,” alisema.
 
Tangu tarehe 21 Mei hadi 19 julai 2012,mteja aliye download  nyimbo yoyote mpya ya Tigobeatz  kwa kuchagua namna mbalimbali za kumwezesha mteja kudownload wimbo kama: kubonyeza alama ya  nyota (*) wakati wanapowapigia ndugu, jamaa au rafiki zao,  kwa kutuma  herufi ya wimbo wowote kwenda 15050, au kwa kupiga 15050 na kununua wimbo wanaoupenda anakuwa tayari amejiingiza katika droo hiyo. Wateja watajiongezea nafasi ya kushinda kwa kila wimbo watakaokuwa wana-udownload.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI