NIMECHAGUA KUWA MKIMBIZI KATIKA MKOA WANGU

Mmiliki wa mtandao huu Bw.Francis Godwin (kushoto) akitoka kujisalimisha polisi akiwa na mkewe Vumilia Mwangosi (kulia) ambaye ni dadake na marehemu Daudi Mwangosi
Hapa mzee wa matukio daima akiwa na mkewe katika basi
Maisha ni safari ndefu yenye misukosuko mingi ila katika maisha ukichagua kuwa mkweli kifo kwako ni rafiki wa karibu sana.

Daudi Mwangosi ameuwawa kwa kusimamia ukweli na kutimiza wajibu wake kama mwanahabari ,leo mimi nalazimika kukimbia mkoa wangu wa Iringa ambao nilitokea kuupenda zaidi kutokana na kusimamia ukweli juu ya kifo cha mwenyekiti wangu katika klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa ,pia kama shemeji yangu na tatu kama mwanaharakati wa kweli katika kutetea wanyonge .

Ila cha kushangaza mbali ya kuwa mimi si muuaji wa Daudi Mwangosi jeshi la polisi wameanza kuniwinda mimi kama shuhuda wa tukio badala ya kuwasaka wauwaji kweli inanishangaza sana ila ndio Tanzania yetu .

Hivyo kutokana na kuendelea kufuatwa fuatwa usiku na mchana binafsi nimechangua kuwa mkimbizi katika mkoa wangu huku nikisimamia ukweli ule ambao ninao na kamwe sitakubali kusema uongo kwa kile nilichokiona nawapenda sana wana Iringa na kuamua kuukimbia mkoa si kwa ajili ya kuwakimbia wakazi wa mkoa wangu nimeamua kwenda mafichoni kwa muda ili kupisha wenye roho mbaya kutaka kunitoa uhai wangu kabla ya kutoa ushahidi wangu.

Iwapo nitapata nafasi zaidi nitaanika kila kitu hapa ili kukuwezesha wewe mdau kujua kilichotokea hadi leo kukimbia mkoa.
Chanzo. FRANCIS GODWIN BLOG

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI