PICHA YETU YA LEO IKIWA NA MSEMO WA KIHAYA WENYE BUSARA NA MAANA KUBWA NDANI YAKE

Kupitia picha yetu ya leo bukobawadau blog tunaendelea kuwaomba ushirikiano wa kimawazo,pia tusaidiane kuwaelewesha ndugu zetu wengine kuitembelea blog yetu na mwenye uwezo tunaomba atusaidie vitendea kazi,na ili tuendele zaidi tupatieni matangazo yenu tuweze tuboresha utendaji wetu!!!. Chanzo. BukobaMdau Blog

CAMERA YETU NDANI YA HOSPITALI YA MKOA

Camera yetu inaangaza Hospitali ya Mkoa wa Kagera, Mkoa wenye jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 246, zikiwemo hospitali 13, Vituo vya afya 23na zahanati 210.
Inaonyesha huduma zinaendelea kama kawaida na hali ya mazingira si mbaya kabisa na kwa kupitia tovuti ya Mkoa inaseme; MKOA wa Kagera kama ilivyo mikoa mingine ya Tanzania unaendelea kutoa ... Huduma kwa Watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi .... wazee wanaofika hasa katika Hospitali hii ya mkoa
Jitiada zetu za kuonana moja kwa moja na Idara zinayotoa huduma katika hospital yetu
kuanzia Utawala, usimamizi mpaka idara ya ODP kwa wagonjwa wa nje hazikufanikiwa ndipo bukobawadau tukaendelea kufanya kile kinachoweza kuonekana kwa siku ya leo.
Camera yetu inaangaza kwa kina na kuona hali halisi ndani ya wodi maalumu ya akinamama wajawazito kama inavyoonyesha wengine ulazimika kulala chini.
Hapa swali moja tunaendelea nalo tatizo ni wodi za kulaza wagonjwa hama tatizo ni vitanda...?!
Tathmini ya haraka haraka inaonyesha katika mkoa wetu wa Kagera asilimia 90 ya hospitali zinazotoa huduma ya TIBA ni za taasisi za dini ikilinganisha na Serikali yenye hospitali moja tu ambayo ni hii ya mkoa iliyopo mjini hapa!!!

SHEREHE ZA KULITABARUKU KANISA KATOLIKI JIMBO LA BUKOBA MJINI BAADA YA UKARABATI MKUBWA ULIOCHUKUA MIAKA 17 KUFANYIKA 7/10/2012 NA MAZISHI YA MAREHEMU MWADHAMA KARDINAL RUGAMBWA NI 6/10/2012

Shughuli ya kuzika masalia ya mwili wa Mwadhama Kardinali Laurean Rugambwa ambaye alikuwa Kardinali wa kwanza mwafrika itafanyika rasmi katika Kanisa la Jimbo Katoliki la Bukoba tarehe 6/10/2012 ikiwa ni miaka 15 tangu alipozikwa kwa muda katika kanisa la Kashozi.
Tarehe 7/10 /2012 kutafanyika sherehe za kulitabaruku Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba Mjini baada ya ukarabati mkubwa uliochukua miaka 17.Shughuli ya kuzikwa upya kwa masalia ya Marehemu Kardinali Rugambwa itakwenda sambamba na sherehe za kuadhimisha miaka 100 tangu kuzaliwa kwake.
Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa,aliyekuwa Kardinali wa kwanza Mtanzania na Mwafrika alifariki dunia 8/12/1997 na kuzikwa tarehe 17/12/1997 kwa muda katika Kanisa Katoliki lililopo Kashozi Wilaya ya Bukoba Vijijini kutokana na ukarabati uliokuwepo katika kanisa hili pichani na sasa unakamili ni Kanisa la Jimbo Katoliki Bukoba.
Marehemu Mwadhama Kardinali Laurean Rugambwa alizaliwa tarehe 12/7/1912 katika eneola Rutabo Kamachumu Wilaya ya Mulebwa na alikuwa Padri 12/12/1947 na aliteuliwa kuwa Kardinali 23/3/1960.

Shughuli hizi zinatarajiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 10,000 kutoka nje ya Bukoba,viongozi mbalimbali pamoja na maaskofu kutoka Ulaya,Kenya,Uganda, Burundi, na mabalozi mbalimbali na viongozi wakuu wa nchi ni sehemu ya Waalikwa!!.

HEKAHEKA ZA HAPA NA PALE BARABARA YA KASHOZI

Hii ni barabara ya kashozi inayokutana na barabara ya kashai ,ni barabara yenye mkusanyiko wa watu wengi ,shughuli nyingi na magari mengi na umaharufu wa barabara hii unazidi kuwepo siku hadi siku ukizingatia ndipo utakapo pita mwili wa Marehemu Cardinal Laurean Rugambwa kutoka parokia ya Kashozi ulipozikwa kwa muda,na kuletwa katika kanisa la jimbo katoliki bukoba, tukio linaloenda kuchukua kasi na kuandika historia mpya katika ukanda huu litakalofanyika tarehe 6/10/2012.Ikiwa ni miaka 15 tangu alipozikwa kwa muda.
Ni barabara moja tegemezi kwa wakazi wa Kashai NHC,kashai halisi ,kilimanjaro,Kisindi,Mafumbo, Kashai Matopeni , Buhembe,kyabitembe, Kahororo, Nyanshenye usawa wa Nyamkazi na vitongoji kadha wakadha...!
Barabara hii nje ya kuwa na shughuli nyingi za kijamii viwanda vya mbao, kiwanda cha samaki cha vic fish,kiwanda cha maji asilia,maghala mbalimbali ya vyakula,Soda na Bia,mashine za kusaga na kukoboa, ,pia inauwelekeo wa shule nyingi za msingi na sekondari.

Pitapita za hapa na pale barabara ya Kashozi.
Sehemu ya raia kuvukia (zebra line)nilichokiona hapa bado watu wanatakiwa kuelimishwa juu ya matumizi yake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.